Waziri Ndumbaro awataka Mawakili kuwa waadilifu

Waziri wa Katiba na Sheria Dkt Damas Ndumbaro


Na Queen Lema, Arusha

Waziri wa katiba na sheria Dkt. Damas Ndumbaro   amewataka mawakili kuwa waadilifu katika utendaji wao wa kazi na kuepuka rushwa.


Dkt. Ndumbaro ameyasema hayo Leo jijini Arusha wakati akifunga mafunzo ya siku nne ya mawakili wa serikali.


Amesema endapo kutakuwa na uadilifu katika utendaji kazi wao wa kila siku utasaidia kufanya Kazi zao kwa umakini.


Amewataka mawakili kutambua kuwa Wana wajibu wa kuheshimu sheria ikiwa ni pamoja na kipambana na  vitendo vya rushwa.


Naye   wakili mkuu wa serikali Gabriel Malata akitoa hotuba yake kwa waziri amesema kuwa pamoja na mafanikio lakini bado wana changamoto ya mawakili kutopata mafunzo maalum yanayoendana na uchumi wa Sasa


Malata ameongeza kuwa baada ya mafunzo hayo mawakili hao wameiva na wataleta Chachu katika kuhakikisha maslahi ya Taifa yanalindwa ipasavyo.


Akitoa shukrani  kwa niaba ya mawakili walioshiriki mafunzo hayo wakili Yesaya Mahenge kutoka mkoani Singida amesema kuwa mafunzo waliyoyapata juu ya namna yankuwndesha mashauri na mengineo yatawasaidia kufanya kazi kwa ufanisi na kuahidi kuwa ni hazina kubwa waliyoipata

This is received, thanks for your comments, will come back to you

Previous Post Next Post