JAMII YATAKIWA KUJITOKEZA KUPINGA UKATILI WA WATOTO

 Na Magesa Magesa,Arusha


JAMII imetakiwa kuhakikisha kuwa  inajikita kikamilifu katika kupinga vita vitendo vya ukatili kwa watoto,badala ya kuliacha jukumu hilo kwa Serikali na mashirika yasiyo ya kiserikali pekee

Katibu tawala wa mkoa wa Arusha,Dkt.Athumani Kihamia ameyasema hayo jana alipokuwa akifungua semina ya siku moja kwa wanahabari iliyolenga kuwajengea uwezo na kuwakumbusha wajibu wao katika kupinga vita
ukatili kwa watoto.

Semina hiyo ilienda sambamba na maadhimisho ya siku ya Mtoto Afrikayanayolenga kupinga ukatili kwa watoto ambayo kilele ni juni 16 mwaka huu huku kaulimbiu ikiwa ni tuimarishe ulinzi wa mtoto,tokomeza ukatili dhidi yake,jiandae kuhesabiwa

‘’Kwa muda mrefu mmekuwa mkiripoti matukio mbalimbali katika vyombo vyenu vya habari ilihali suala la ukatili kwa watoto hamlipi kipaumbele,hivyo wakati umefika mhakikishe kuwa mnajikita zaidi katika kuripoti matukio ya ukatili kwa watoto”alisisitiza.

Katibu Tawala huyo ambaye ndiye Mwenyekiti wa kamati ya kupinga ukatili kwa watoto Mkoani hapa alisema kuwa matukio mengi ya ukatili kwa watoto yamekuwa yakichangiwa na mtafaruku katika familia hali inayopelea wazazi kutendana na kukuta mtoto kukosa mwelekeo na kujiingiza mtaani hali ambayo hupelekea kufanyiwa ukatili.

“Matukio kama ukeketaji,ubakaji,ulawiti,ndoa na mimba za utotoni,watoto kunyimwa haki yao ya kuishi na kupata elimu yamekuwa yakiongezeka sana katika jamii,hivyo wakati emefika jamii kwa ujumla kupaza sauti na kuwafichua wale wote wanaojihusisha na vitndo hivyo.

Kwa upande wake Diwani wa kata ya Ngarenaro,jijini hapa Isaya Doita alisema kuwa ukatili kwa watoto imekuwa ni adha kubwa sana hususani Mkoani hapa  na kuongeza kuwa wale wote wanajihusisha na vitendo vya uakatili kwa watoto ni sawa na wauaji.

Naye mkurugenzi wa Shirika lisilo la Kiserikali la Center for Woman,Children anda Youth Developmend(CWCD)  Hindu Mbwego,amesema kuwa baadhi ya walezi na wazazi wamekuwa ni chanzo cha ukatili huo kwa kushidwa kusimamia kikamilifu jukumu la kuwalea watoto wao.

Aliimba serikali kuhakikisha kuwa inarekebisha baadhi ya sheria kwani zimekuwa zikichangia ukatili kwa watoto ikiwemo Sheria ya ndoa na kuongeza kuwa pamoja na kuwa dhamana ni haki ya kila mtu ila wakati
umefika kuangalia suala la dhamana kwa wale wote wanabainika kujihusisha na vitendo vya ukatili kwa watoto.

This is received, thanks for your comments, will come back to you

Previous Post Next Post