Na Magesa Magesa,Arusha
KIONGOZI wa mbio za Mwenge Kitaifa Sahili Nyanzabara
Geraruma,amewahimiza wananchi Mkoani hapa kuhakikisha kuwa wanajitokeza kwa wingi katika zoezi la sensa ya watu na makazi inalotarajiwa kufanyika Agosti 23 mwaka huu.
Aliyasema hayo jana katika mbio za Mwenge wa uhuru wilayani hapa, na kuwataka kila mmoja kuhakikisha anahesabiwa ikiwa ni pamoa na kutoa taarifa sahihi zitakazoiwezesha serikali kupanga mambo ya kimaendeleo.
Kadhalika Geraruma aliwataka wananchi hususani vijana kuacha kujiingiza katika matumizi ya dawa za kulevya, kunnywa pombe kupindukia pamoja na kujiepusha na vitendo vya ngono zembe.
“Suala la utumiaji wa madawa ya kulevya,unjwaji pombe wa kupindukia limekuwa likiongezeka kadiri siku zinavyosonga mbele hususani kwa vijana, hivyo ninawashauri kuachana na matumizi hayo ya madawa na badala yake wajikite katika kufanya kazi ili kujiongezea kipat wao binafsi pamoja na familia zao”alisisitiza.
Kiongozi huyo wa mwenge pia aliwashauri wananchi kujitokeza mara kwa mara kupima afya zao katika vituo vya kutolea huduma za afya ili kubaini kama ana tatizo linalomsumbua na kuweza kuchukua hatua mapema
kuliko kusubiri hadi tatizo linakuwa sugu.
Aliwaonya viongozi wote wa serikali wanaotumia vibaya madaraka yao ikiwamo wale wabadhirifu wa fedha za miradi ya maendeleo na kwamba serikali itawachukulia hatua za kinidhamu ambapo pia amewataka kusimamia kikamilifu miradi yote inayotekelezwa katika maeneo yao.
Kadhalika aliitaka jamii kuwa wazalendo na kuachana na vitendo vya kutoa na kupokea rushwa ikiwa ni pamoja na kuwataka wazazi au walezi kuhakikisha kuwa wanasimamia makuzi ya watoto wao
Awali akipokea Mwenge huo wa uhuru kutoka wilayani Monduli,Mkuu wa Wilaya ya Arusha,Said Mtanda alisema kuwa Mwenge huo utakimbizwa kilometa 98.1katika Wilaya ya Arusha ambapo utazidua miradi saba ya maendeleo yenye thamani ya shilingi bilioni 3.4.
Mkuu huyo wa Wilaya aliwataka wananchi wote ambao miradi hiyo imetekelezwa katika maeneo yao kuhakikisha kuwa wanaitunza kikamili ili idimu kwa muda mrefu kwa manufaa ya sasa na ya kiazi kijacho.
“Natoa onyo kwa wale wote wanaohujumu miundombinu ya mradi kwa kuiba vifaa au kuhujumu kwa namna yeyote ile serikali haitasita kumchukulia hatua kali za kinidhamu hivyo nitoe rai kwa wananchi huhakikisha kuwa Inawafichua wale wote wanaohujumu miradi ya maendeleo”alisema Mtanda
Mwenge wa Uhuru ukiwa Wilayani hapa ulizindua miradi saba ya maendeleo
katika maeneo tofauti jijini hapa ikiwa ni katika sekta za
afya,maji,elimu na barabara.