DC AJITOLEA KUMSOMESHA MWANAFUNZI ALIYEJITOLEA UTENDAJI KIJIJI CHA MTANGA NJOMBE

Mkuu wa Wilaya ya Njombe Kissa Gwakisa
Mwanafunzi Alex Msambwa 

Na Mwandishi Wetu,  NJOMBE 

Mkuu wa wilaya ya Njombe Kissa Gwakisa Kasongwa amejikuta katika simanzi na kuahidi kugharamia masomo ya mkazi mmoja wa Kijiji Cha Mtanga anaefahamika kwa jina Alex Msambwa ambaye amejitolea kwa moyo mkunjufu utendaji wa kijiji hicho kwa zaidi ya miaka 12 bila kulipwa mshahara

 

Mkazi huyu mwenye elimu ya kidato cha nne imekuwa ngumu kwa Halmashauri ya mji wa Makambako kumpa ajira ya kudumu kwasababu ya kukosa sifa ya kielimu licha ya kufanya kazi kwa kiwango Cha juu katika kipindi chote anachojitolea.

  

Kijiji Cha Mtanga kilichopo zaidi ya km 30 kutoka kitovu Cha mji wa Makambako kimetajwa kuwa na changamoto nyingi zinazokwamisha maendeleo Ikiwemo ya Ukosefu wa mtendaji anaetambuliwa na kupata Ajira rasmi na serikali jambo ambalo baadhi ya wananchi wanaamini ndiyo chanzo kikuu Cha kuchelewesha Kasi ya ukuaji wa  Kijiji Chao katika nyanja mbalimbali.

 

Akiwa katika muendelezo wa ziara yake ya kikazi ya Kijiji kwa Kijiji ya kusikiliza kero za wananchi na kuzipa ufumbuzi mkuu wa wilaya ya Njombe amepokea kero ya mkazi huyu aliyetumikia serikali kwa miaka isiyopungua 10 kwa kujitolea na Kisha kuguswa na changamoto hiyo.

  

Ombi halo la wananchi la kumpa Ajira ya kudumu mkazi huyo ama kuleta mtendaji mwenye sifa linamgusa mkuu wa wilaya ya Njombe Kissa Gwakisa Kasongwa na Kisha kuahidi kumpa pesa ili akasome chuo huria na huku akimpa agizo mkurugenzi wa Halmashauri kumpa kipaumbele cha ajira pindi atakapomaliza masomo hata kwa ngazi ya cheti

  

Akitoa hisia zake kwamsaada wa kimasomo aliyopewa na mkuu wa wilaya kijana Alex Msambwa anasema mwanzo alikuna na changamoto nyingi ikiwepo ya kupuuzwa kwasababu ya kiwango Cha elimu na kudai kwamba pamoja shida hiyo alipiga moyo konde kwa kuendelea na kazi hivyo fursa aliyopewa anaitumia ipasavyo.

  

Akiwa Kijiji Cha Mtanga mkuu wa wilaya amepokea changamoto nyingine  za maji,umeme huku katika Kijiji Cha Ibatu changamoto kubwa ikitajwa kuwa ni barabara.

This is received, thanks for your comments, will come back to you

Previous Post Next Post