Wawekezaji Kutoka Falme za Imarate Watua Njombe Kuwekeza Viwanda vya Nyama,Kilimo cha Parachichi na Mradi wa Farasi Katika Eneo Lenye Ukubwa wa Ekari 100,000

 NA MWANDISHI WETU, NJOMBE 


Ikiwa siku chache zimepita tangu rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan afanye ziara ya kikazi katika nchi ya OMAN ,Tayari mkoa wa Njombe umeanza kuonja matokeo chanya ya ziara hiyo ambapo umepokea ugeni kutoka falme za Imarate uliyoambatana na kampuni ya Kitanzania ya BACOIN ya mkoani Morogoro inayomilikiwa na familia ya bilionea Sarah Bamatraf na mwanae Murad Bumatraf ambao umelenga kununua ardhi ekari 100,000 kwa ajili kuanzisha kilimo cha parachichi,Viwanda vya Nyama pamoja na mradi wa farasi ili kutanua wigo wa vivutio vya utalii.

Ugeni huo ambao umeambatana na mbunge wa africa mashariki umesema umeshawishika kuja kuwekeza Tanzania hususani katika mkoa wa Njombe kwasababu ya uwepo wa mazingira rafiki ya uwekezaji kwasasa na kwamba umechagua Njombe kutokana na kuwa hali ya hewa rafiki kwa miradi hiyo.

Kabla ya kutembelea mashamba ya wakulima wa parachichi msafara huo umeripoti katika ofisi za mkuu wa mkoa wa Njombe na kupokewa na katibu tawala wa mkoa huo Judica Omary ambapo kwa mkuu wa mkoa akasema serikali ya mkoa huo ipo tayari kupokea uwekezaji huo na kisha kuahidi kutoa ushirikiano wa hali ya juu ikiwa ni pamoja na kusaidia kupatikana kwa ardhi inayohitajika kwa ajili kuanzisha miradhi mikubwa ya kilimo,viwanda na utalii wa farasi.

“Nia ya uwekezaji wa hawa wageni ni kupata ekari 100,0000 hivyo tuna jukumu la kutafuta ardhi hiyo katika maeneo mbali mbali,tutafanya kila namna ipatikane kwasababu wameonyesha nia ya dhati ya kuwekeza katika mazao tofauti”amesema Judica Omary

Awali mbunge wa Afrika Mashariki Fancy Nkuhi ambaye ameambatana na timu hiyo amesema kasi ya uongezeko la watalii na wawekezaji kwasasa nchini imetokana na matunda ya ziara ya rais nchini Omani na filamu ya "The Royal Tour ambayo imefanywa na rais Samia na kuzinduliwa kwa kutazamwa katika mataifa tofauti ulimwenguni

“Nimekuja na wageni ambao wanatoka nchi za falme za kiarabu ambao wameonyesha nia ya kuwekeza kwenye zao la Parachichi kwenye mkoa wa Njombe,huu ni muendelezo wa kazi kubwa aliyoifanya Mh,Rais kwenye Ziara yake na filamu ya Royal tour”alisema Nkuhi

Miongoni mwa wakulima wakubwa wa parachichi waliotembelewa na wawekezaji hao ni Steven Mlimbila maarufu Nemes ambae anasema licha ya kuyumba kwa soko la parachichi kwa muda lakini wanafurahishwa na jitihada za serikali za kuendelea kutafuta wawekezaji katika kilimo hicho na viwanda vya kuongeza thamani ya mazao ya matunda na nyama kwani kupitia hilo zinatengenezwa ajira.

"Sisi kama wakulima wa parachichi wa mkoa wa Njombe ,tunaishukuru serikali kwa kuendelea kuwapigania wakulia kwa kutafuta wawekezaji na nipende kuwatoa hofu juu ya soko ambalo lilitetereka siku chache zilizopita ,Alisema Setev Mlimbila . 

This is received, thanks for your comments, will come back to you

Previous Post Next Post