Waandishi Arusha waazimia kuonana na IGP

Waandishi wa habari wa Arusha wakifuatilia mada kuhusu ulinzi na usalama

Mratibu wa APC Seif Mangwangi akiandika maazimio ya mdahalo huo
Washiriki wa mdahalo kuhusu ulinzi na usalama wakitoa maazimio
Washiriki wa mdahalo kuhusu ulinzi na usalama walimsikiliza mwezeshaji
Makamu Mwenyekiti wa APC Mussa Juma

 Na Mwandishi Wetu Arusha

Chama cha waandishi wa habari Mkoa wa Arusha kimesema kitaendelea kufanya ushirikiano na jeshi la Polisi licha ya viongozi wa jeshi hilo kutokuwa karibu na waandishi wa habari.


Akizungumza wakati wa ufunguzi wa mdahalo kuhusu ulinzi na usalama jana Jijini Arusha,  Makamu Mwenyekiti wa APC Mussa Juma amesema lengo la mdahalo huo ni waandishi wa habari kukutana na jeshi la polisi kwaajili ya kujenga mahusiano lakini viongozi wa Polisi Arusha wamekuwa wakishindwa kufika.


Juma amesema wakati wa maandalizi ya mkutano huo, jeshi la polisi lilishirikishwa kwa kupelekewa mwaliko na walithibitisha ushiriki wao ikiwa ni pamoja na kutoa mada lakini hadi mafunzo hayo yanafunguliwa jana walikuwa hawajatokea.


" Tumeshindwa kuelewa lengo la Polisi ni nini, kwa kuwa hii ni mara ya tatu tunawaalika kwenye mdahalo na tumekuwa tukiwaeleza kabisa lengo letu ni nini, mwisho tumeshaandaa kila kitu wao hawatoki, itabidi mwishoni tuwe na maazimio ya nini kifanyike"alisema Juma.


Awali mratibu wa Arusha Press klabu,Seif Mangwangi alisema walitarajia polisi kufika katika mjadala huo alipeleka barua rasmi nakuzungumza na viongozi hao 


"Nadhani Kuna changamoto ya ndani ndio sababu tutaomba usaidizi zaidi Kwani tayari Mkuu wa mkoa Arusha na Mkuu wa wilaya waliingilia kati hii sintofahamu lakini bado Kuna changamoto"alisema 


Wakichangia katika mdahalo huo waandishi wa habari waliutaka uongozi wa APC kuwasiliana na sekretarieti ya UTPC na kuona uwezekano wa kuwasiliana na viongozi wa juu wa jeshi la Polisi Nchi.


Katibu Mkuu wa APC Zulfa Mfinanga alisema ni muhimu jambo hilo kupatiw Suluhu mapema ili kurejesha mahusiano baina ya waandishi na jeshi la polisi Arusha.


" Huu sasa ni utani, mara ya mwisho RPC alituita na kutuomba msamaha, na akasema wazi atakuwa na ushirikiano na waandishi kwa jambo lolote tutakaloandaa, wakati tunaandaa mdahalo huu amepigiwa simu hakupokea, baadae tukaamua kuwasiliana na OCD ambaye yeye alithibitisha kushiriki na barua alipewa, mwisho wa siku ameshindwa kutokea kwa madai ya kupata vikao vya ghafla," alisema  Mfinanga


Mwandishi Novatus Makunga alishauri kufanyika vikao zaidi na viongozi wa polisi ili kuondoa changamoto ambazo zinajitokeza katika mkoa Arusha.


Awali akitoa mada kuhusu ulinzi na usalama, mtaalam wa masuala ya mtandao Elie Chansa alisema waandishi wa habari wanatakiwa kujua mbinu mbalimbali za matumizi ya mitandao ili kuwaepusha na hatari ya kuumizwa na watu wabaya.


Amesema endapo waandishi wa habari watashindwa kujua mbinu hizo ni rahisi taarifa zao kudukuliwa na watu wenye nia ovu na matokeo yake ni kuhatarisha usalama wao.


Chama Cha waandishi wa habari mkoa Arusha Kwa kushirikiana na umoja wa vilabu vya waandishi wa habari nchini(UTPC) wapo katika mradi wa ulinzi na usalama Kwa wanahabari ambao unafadhiliwa na shirika la kimataifa la IMS.


Katika mradi huo kumekuwa na midahalo baina ya wanahabari na jeshi la polisi ili kuboresha mahusiano na kuondoa migogoro isiyo ya lazima.

This is received, thanks for your comments, will come back to you

Previous Post Next Post