Afariki kwa moto akiwa ndani

 

Na Mapuli Misalaba, Shinyanga 

 Mwanaume mmoja mkazi wa mtaa wa Luhende kata ya Masekelo Manispaa ya Shinyanga, Bwana Ngelela Seleli mwenye umri wa miaka zaidi ya 40 amefariki Dunia akisadikika kuungua moto akiwa ndani ya chumba chake cha kulala. 

 Mwandishi wetu amefika kwenye eneo la tukio na kuzungumza na Mwenyekiti wa mtaa wa Luhende Msafiri Nadula ambaye amesema tukio hilo limetokea leo Septemba 7,2022 majira ya saa nane usiku na kwamba mwenyekiti Nadula amesema amepata taarifa hizo kutoka kwa wananchi wa mtaa huo.


Nadula ameeleza kuwa marehemu Ngelela Seleli alikuwa na ugongwa wa kifafa ambapo pia alikuwa ni mjasiliamali mdogo akijishughulisha na biashara ya kuuza vifaa mbalimbali ikiwemo vyuma chakuvu. “Mimi nimefika kwenye tukio nikakuta wananchi wanajitihada za kuuzima moto lakini tulipoangalia alimokuwa amelala alikuwa tayari ameungua kabisa mwili wote ikabidi nipige simu polisi ndiyo wamekuja kuuchukua mwili”. 

 “Lakini pia marehemu alikuwa na ugonjwa wa akili japo alikuwa anajitambua na alikuwa anafanya biashara yake vizuri na kodi alikuwa analipa mwenyewe”. amesema Mwenyekiti Nadula

 
Wakizungumza baadhi ya wananchi walioshuhudia tukio hilo wameeleza namna walivyoguswa na msiba wa marehemu Ngelela Seleli ambaye alikuwa ni mpangaji katika nyumba ya Khadija Issa marufu kwa jina la Mama Said. 


Mwandishi wetu pia amefika katika Hospitali ya rufaa ya Mkoa wa Shinyanga na kuzungumza na mganga mfawidhi Dkt. Luzila John ambaye amekili kuupokea mwili wa marehemu huyo majira ya saa kumi na moja asubuhi. 
 “Mnamo saa kumi na moja alfajiri tulipokea mwili wa marehemu ambaye alikuwa amesadikika kuungua moto anaitwa Ngelela Seleli wa kiume ambaye sisi tulimpokea akiwa tayari ameshafariki kwahiyo tulithibitisha kifo”.amesema Dkt. Luzila


Kwa upande wake kamanda wa jeshi la polisi Mkoa wa Shinyanga kamishna msaidizi wa polisi Janeth Magomi amethibitisha kutokea kwa tukio hilo huku akisema jeshi hilo linaendelea na jitihada za kufanya uchunguzi ili kubaini chanzo cha tukio.


 “Kwanza nathibitisha kutokea kwa tukio hilo nimefika kwenye tukio na nimezungumza na ndugu wa marehemu kwamba huyu aliyefariki Dunia kwa kuungua na moto kile chumba alichokuwa akilala kinauchafu uchafu, kina makaratasi, machuma niliwauliza ndugu zake na marehemu kuwa huyu ndugu yenu alikuwa akilala hapa wakasema ndiyo” “Lakini ndugu yake na huyu marehemu ambaye ni mdogo wa marehemu anaitwa Japhar Seleli amesema Ngelela alikuwa anafanya shughuli za kuokota chupa lakini pia alikuwa na ulemavu wa akili chanzo bado hatujajua lakini jeshi la polisi tunaendelea kupeleleza ili kujua chanzo”. Amesema kamanda Magomi IMG_20220907_063239_646 - Copy.jpg IMG_20220907_063305_737 - Copy - 

This is received, thanks for your comments, will come back to you

Previous Post Next Post