Sido yatoa elimu ya ujasiriamali kwa vijana 130 Arusha

Vijana wajasiriamali na wenye ndoto za kumiliki viwanda wakifuatilia mada za umiliki wa viwanda jana
Picha ya kwanza ni viongozi wa Sido mkoa wa Arusha,makatibu tawala mkoa wa Arusha,pamoja na mmiliki wa kiwanda wakitetea jana kwenye ufungaji wa programu ya mafunzo ya uanagenzi kwa vijana 130 wa mkoa wa Arusha
Meneja wa Sido Mkoa wa Arusha Jaffar Donge in


Na Mwandishi Wetu, Arusha

Vijana 130 kutoka maeneo mbalimbali ya jiji la Arusha wamefanikiwa kupatiwa elimu ya ujasiriamali pamoja na namna ya kujiajiri kwenye sekta ya viwanda


Vijana hao wamefanikiwa kupatiwa elimu kupitia mradi wa uanagezi ambapo mradi huo uliibuliwa na Wizara ya elimu sayansi na teknolojia na kudhamiwa na Benki ya dunia Huku ikiratibiwa na SIDO



Akiongea na vyombo vya habari mapema jana mara baada ya kufungua mradi wa uanagezi ambao uliwakutanisha wamiliki,pamoja na vijana wajasiriamali mkoa wa Arusha meneja wa Sido mkoa wa Arusha Bw Jafari Donge alisema kuwa mradi huo ulidumu kwa kipindi Cha mwezi mmoja 


Donge alisema kuwa  Sido kupitia kwenye mradi huo umeweza kuibua ajira mpya kwa kuwa vijana hao waliweza kupelekea kwenye viwanda mbalimbali ambavyo vinatekeleza majukumu Yao ya kiujasirimali


"Vijana Hawa tuliwapeleka kwenye viwanda mbalimbali kama vile viwanda vya usindikaji,saluni,gereji,masuala ya mtandao,mikate,uhandisi,utalii Hawa wamiliki wote wapo chini ya Sido na tunashukuru sana wamewapokea kwa muda mfupi wa mwezi mmoja na tayari wameshapata mafunzo  Huku wengine wakipata ajira za kudumu"aliongeza 


Katika hatua nyingine aliwaasa vijana kuhakikisha kuwa wanatafuta fursa mbalimbali ambazo zinatangazwa ingawaje bado Kuna changamoto ya uhaba wa ajira 


Pia aliomba wadau kama vile wizara husika kuweza kutoa fursa sanjari na kuibua miradi kama huo hata kama utadumu kwa muda mfupi ili kuweza kuwasaidia vijana kuanzisha na kumiliki viwanda vidogovidogo 


Mmoja wa wamiliki wa viwanda Bi Salma mnaro aliweza kuishukuru waandaji wa mpango huo pamoja na Sido kwa kuweza kuwateua vijana ambao walikuwa na uitaji mkubwa wa ajira na hawana uwezo wa kupata uzoefu wa kumiliki viwanda 


Salma aliongeza kuwa ni muhimu sana kuishukuru Serikali lakini pia Sido kwa kuwa wamekuwa matendo chanya ambayo wameweza kufungua milango kupitia hata taasisi za fedha 


Alihitimisha kwa kuwataka vijana hao ambao muda si mrefu wanaanzisha viwanda vyao kuhakikisha kuwa wanasimama ipasavyo katika ndoto zao za kumiliki pamoja na kusimama katika ubora wa bidhaa ili waweze kuteka soko la dunia.

This is received, thanks for your comments, will come back to you

Previous Post Next Post