Na Mapuli Misalaba,
Shinyanga
Katibu wa kampeni ya
Shujaa wa Maendeleo na Ustawi wa Jamii Tanzania SMAUJATA Mkoa wa Shinyanga
Bwana Daniel Kapaya ametoa shukurani zake kwa kuteuliwa kutumikia nafasi hiyo
huku akiahidi kutekeleza majukumu yake kwa mujibu wa taratibu zilizopo pamoja
na kushirikiana na viongozi wengine.
Bwana Kapaya amemshukuru
Mwenyekiti wa wa SMAUJATA Taifa shujaa Sospeter Bulugu kwa kumteua kuwa sehemu ya
mashujaa wanaopinga ukatili kupitia nafasi hiyo ya katibu wa SMAUJATA Mkoa wa
Shinyanga.
Katibu wa SMAUJATA Mkoa
wa Shinyanga Bwana Daniel Kapaya amemshukuru waziri wa maendeleo ya jamii,
jinsia, wanawake na makundi maalum Dkt. Dorothy Gwajima kwa kuendelea kutambua
mchango unaofanywa na kampeni ya SMAUJATA.
Pia ametumia nafasi hiyo
kumshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan
pamoja na viongozi wengine wa serikali kwa kuungana pamoja kukataa vitendo vya
ukatili Nchini.
Aidha amemshukuru na
kumpongeza Mwenyekiti wa SMAUJATA Mkoa wa Shinyanga Bi. Nabila Kisendi jina
maarufu Madam Kisendi na viongozi wengine wa Mkoa huo kwa kumwamini katika
nafasi hiyo ambapo ameahidi kutoa ushirikiano wa dhati katika hatua za
kutokomeza ukatili Mkoani Shinyanga.
“Nashukuru
sana kwa uteuzi wa Tarehe 24 Mwezi wa sita Mwaka huu 2023 kwanza kabisa nianze
kumshukuru Mwenyekiti wangu ngazi ya Taifa Shujaa Sospeter Bulugu kwa kuniona
na mimi kijana nafaa ambaye naweza kuchapa kazi nikiwa katibu wa Mkoa na mimi
nitanya kazi kwa juhudi ili kuhakikisha tunapunguza au kumaliza kabisa ukatili,
lakini pia nimshukuru waziri mwenye dhamana mama yetu Dkt. Dorothy Gwajima kwa
kutambua mchango wetu sisi vijana”. Amesema Daniel Kapaya
“Lakini
pia nimshukuru Mwenyekiti wangu wa Mkoa wa Shinyanga Madam Kisendi na
waandamizi wengine nikiwa katibu wa SMAUJATA Mkoa nitashirikiana nao kwa karibu
katika kufanya kazi hii kwa sababu tusipokuwa na ushirikiano maana yake
tutashindwa kutokomeza ukatili, niseme tu kuwa nitajitahidi sana kuanzia ngazi
ya Mkoa, Wilaya, kata, matawi mpaka watu wa chini kabisa tutawafikia ili kuibua
ukatili unaoendelea kufanyika”. Amesema Daniel Kapaya
Mwenyekiti wa SMAUJATA
Taifa shujaa Sospeter Bulugu alimteua Bwana Daniel Kapaya kuwa katibu wa SMAUJATA
Mkoa wa Shinyanga tangu Jumamosi Juni 24,2023.
SMAUJATA ni kampeni ya kupinga ukatili Nchini iliyoanzishwa Mwaka jana chini ya Waziri wa maendeleo ya jamii, jinsia, wanawake na makundi maalum Dkt. Dorothy Gwajima kwa kushirikiana na Mwenyekiti wa SMAUJATA Taifa Bwana Sospeter Mosewe Bulugu.