SMAUJATA SHINYANGA YAZINDUA BONANZA LA KATAA UKATILI CHEUPE CUP KUFANYIKA SIKU 6 MTAA WA DOME

Na Mapuli Misalaba, Shinyanga

Kampeni ya Shujaa wa Maendeleo na Ustawi wa Jamii Tanzania SMAUJATA Mkoa wa Shinyanga leo imezindua bonanza la kupinga ukatili linalokwenda sanjari na michezo mbalimbali katika Mtaa wa Dome kata ya Ndembezi Manispaa ya Shinyanga.

Bonanza hilo linalokwenda kwa jina la Cheupe Cup limezinduliwa leo Jumanne Juni 27,2023 kwa kushirikiana na Mwenyekiti wa mtaa wa Dome Bwana Solomon Najulwa jina maarufu Cheupe ambalo litafanyika kwa siku sita (6).

Akizindua Bonanza hilo makamu Mwenyekiti wa SMAUJATA Mkoa wa Shinyanga Mwalimu Vicent Kanyogota amekemea ukatili unaofanyika mitaani huku akiwaomba wananchi kutoa taarifa za ukatili kwa kupiga 116 au kufikisha kwa viongozi wa SMAUJATA Mkoa huo.

Mwalimu Kanyogota amesema Kampeni ya SMAUJATA imelenga kutetea haki za kila mtu kwa kuzuia vitendo vya uhalifu ikiwemo vitendo vya ukatili vinavyochangia ukosefu wa amani kwenye familia, jamii na Taifa kwa ujumla.

Amesema SMAUJATA Mkoa wa Shinyanga itaendelea kutetea haki na kuibua vitendo vya ukatili kwa lengo la kujenga jamii yenye mazingira salama katika maisha ya kila siku.

Katibu wa SMAUJATA Mkoa wa Shinyanga Bwana Daniel Kapaya amewasisitiza wazazi na walezi kuimarisha ulinzi wa watoto wao ili kuwaepusha na vitendo vya ukatili.

Baadhi ya wakazi wa mtaa wa Dome waliohudhuria bonanza hilo la Cheupe Cup wameipongeza SMAUJATA Mkoa wa Shinyanga kwa kushirikiana na Mwenyekiti wa mtaa huo ambapo wamesema watahakikisha taarifa zote za ukatili wanazifikisha sehemu sahihi kwa wakati.

Wananchi hao wameiomba SMAUJATA Mkoa wa Shinyanga kuendelea kutoa elimu ya ukatili pamoja na ubunifu huo wa michezo mbalimbali ambapo wamesema kwa kufanya hivyo itasaidia jamii ya Mkoa wa Shinyanga kupaza sauti juu ya ukatili unaoendelea kufanyika.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa mtaa wa Dome Bwana Solomon Nalinga Najuwa jina maarufu Cheupe ambaye pia ni Mwenyekiti kamati ya maadili SMAUJATA Mkoa wa Shinyanga amesema michezo mbalimbali itaendelea kufanyika katika uwanja wa Balina English na kwamba amewakaribisha wakazi wa Mkoa wa Shinyanga kujitokeza kwa wingi kwenye bonanza hilo.

Michezo mbalimbali imefanyika ikiwemo mchezo wa mpira wa miguu pamoja na mchezo wa kuvuta Kamba kwa wanawake ambapo washidi mbalimbali wamepokea zawadi.

Makamu Mwenyekiti wa SMAUJATA Mkoa wa Shinyanga Mwalimu Vicent Kanyogota akizindua bonanza la kata ukatili Cheupe Cup litakalofanyika kwa siku sita kuanzia Juni 27,2023.

Makamu Mwenyekiti wa SMAUJATA Mkoa wa Shinyanga Mwalimu Vicent Kanyogota akizindua bonanza la kata ukatili Cheupe Cup litakalofanyika kwa siku sita kuanzia Juni 27,2023.

 

 





This is received, thanks for your comments, will come back to you

Previous Post Next Post