JESHI LA POLISI MKOA WA SHINYANGA KUENDELEA NA UCHUNGUZI KWA WATU WAWILI WALIOUAWA

Na Mapuli Misalaba, Shinyanga

Jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga linaendelea na uchunguzi wa tukio la kijana anayefahamika  kwa jina la Kulwa Sosoma mwenye umri wa miaka 42 mkazi wa Ibinzamata katika manispaa ya Shinyanga ambaye aliuawa kwa kushambuliwa na watu waliojichukulia sheria mkononi.

Hayo yamebainishwa na kamanda wa jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga kamishna wa Polisi Janeth Magomi ambapo amesema tukio hilo limetokea  Octoba 24 katika kijiji cha Bugayambelele baada ya kushambuliwa na watu waliojichukulia sheria mkononi wakimtuhumu kuhusika na tuhuma za wizi.

Mjomba wa  Marehemu huyo Bwana  Hamis Mathias ameelezea kuwa  chanzo cha kifo cha kijana wao kimetokana na kushambuliwa na watu wenye hasira kali ambao walimtuhumu kuhusika na tuhuma za kuiba mpira wa maji unaotumika kumwagilia Bustani

Aidha jeshi la polisi Mkoa wa Shinyanga limesema bado linaendelea na uchunguzi wa tukio la Mwanaume mmoja  aliyefahamika kwa jina la Tungu Sabuni Tungu mwenye umri wa Miaka 60 mkazi wa kata ya usule Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga ambaye alifariki Dunia baada ya kukatwa panga na Bwana Nkwabi Joseph mkazi wa kijiji hicho.

Tukio hilo limetokeo Oktoba 25,2023 majira ya saa tatu asubuhi kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga kamishina wa polisi Janeth Magomi  amethibitisha kuwa na taarifa za tukio hilo,ambapo amesema Uchunguzi unaendelea ili kubaini waliohusika na mauaji hayo.

Kamanda Magomi ametumia nafasi hiyo kuwaomba wananchi wa Mkoa wa Shinyanga kuendelea kushirikiana na jeshi hilo ikiwemo kutoa taarifa za wahalifu na uhalifu unaojitokeza ili hatua za kisheria zichukuliwe.

 


This is received, thanks for your comments, will come back to you

Previous Post Next Post