RC MNDEME AFANYA ZIARA WILAYA YA KISHAPU, ATOA MAAGIZO KWENYE MIRADI YA MAENDELEO


Na Mapuli Misalaba, Shinyanga

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Solomon Mndeme ameendelea na ziara zake ambapo  Jumatatu Oktoba 30,2023 ametembelea na kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo katika Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu Mkoani Shinyanga.

Mhe. Mndeme pamoja na kupokea taarifa za miradi ya maendeleo amesikiliza na kupokea kero za wakazi wa Wilaya ya Kishapu huku akiwaelezea hatua mbalimbali za maendeleo ya Mkoa wa Shinyanga  ambapo amewaomba kuendelea kuiunga mkono serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika shughuli za maendeleo.

RC Mndeme amekagua ujenzi wa jengo jipya la ofisi ya mkuu wa Wilaya ya Kishapu linalotekelezwa kupitia fedha za serikali zaidi ya Bilioni moja ambapo ametoa wiki mbili mradi huo uwe umekamilika.

Awali katika taarifa ya mradi iliyosomwa na katibu tawala wa Wilaya ya Kishapu Bi. Fatma Mohamed mradi huo upo katika hatua ya ukamilishaji na kwamba ulianza Mwezi Machi 3,2022.

Mhe. Mndeme ametembelea nyumba mpya ya mkuu wa Wilaya ya Kishapu inayojengwa kupitia fedha za serikali kuu ambapo pia ametoa wiki mbili mradi huo we umekamilika ili shughuli za taratibu zingine za maendeleo ziweze kuendelea.

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme katika ziara yake ya leo amekagua ujenzi jengo la huduma jumuishi (One stop Center) katika Hospitali ya Wilaya mradi huo unatekelezwa kwa fedha kutoka Serikali Kuu kwa kushirikiana na shirika la UNFPA.

Mndeme amekagua na kuweka jiwe la msingi katika ujenzi wa mradi wa maji ya ziwa Viktoria Seseko - Ngundangali unaotekelezwa kwa fedha za Serikali Kuu kupitia mradi wa P4R mradi huo unatekelezwa kwa muda wa mwaka  mmoja ambapo   ulianza  kujengwa  Tarehe 30 Machi , 2023  na  unatarajiwa   kukamilika  Mwezi Machi,  2024.

Akisoma taarifa fupi ya mradi huo wa maji ya Ziwa Viktoria Seseko – Ngundangali, meneja wa RUWASA Wilaya ya Kishapu mhandisi Dickson Kamazima ameeleza lengo la mradi huo ambapo amesema wananchi 15,500 watanufaika na mradi huo.

“Muda wa  utekelezaji   Mradi  siku 365  sawa  na  mwaka  mmoja ,  Mradi  ulianza  kujengwa  Tarehe 30 Machi , 2023  na  unatarajiwa   kukamilika  Mwezi Machi,  2024.”

“Lengo la mradi hu ni kumtua mama ndoo kichwani, kwa kumpunguzia umbali wa kufuata maji na kumuongezea muda wa kushiriki shughuli za kiuchumi na kijamii, pia kupunguza magonjwa yanayosababishwa na kutumia maji yasiyo safi na salama”. Amesema mhandisi Kamazima  

“Kazi zilizopangwa kutekelezwa katika Mradi huu, ni ujenzi wa matangi matatu (3) ya kuhifadhi maji yenye ujazo wa lita 200,000 kwenye minara wa mita 15 pamoja  na uzio, kutandaza mtandao wa bomba umbali wa Kilomita 41.5na kujenga vituo vya kuchotea maji (DPs) 31. Kazi zote zimekamilika kwa asilimia 95 (95%)”.

“Gharama ya Mradi ni Tsh 2,810,058,195.00 ikijumuisha Kodi ya ongezeko la Thamani (VAT) ambazo ni fedha kutoka Serikali kuu, kuptia Program ya Malipo kwa Matokeo (Payment for Result), hadi sasa Mkandarasi ameshalipwa   kiasi cha Tsh 330,495,816.25”. Amesema mhandisi Kamazima

“Wanufaika wa mradi huu ni wananchi wa vijiji vitano (5) vya Ngundangali, Dugushilu, Kakola, Seseko na Mpumbula wapatao 15,500”

“Kwa niaba ya Wananchi wa Wilaya ya Kishapu, nachukua fursa hii kuishukuru Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, inayoongozwa na Rais Mhe: DKT Samia Suluhu Hassan kwa jitihada zake za kutupatia fedha za ujenzi wa Miradi ya maji katika Wilaya ya Kishapu”. Amesema mhandisi Kamazima

Mhe. Mdeme amekagua ujenzi wa nyumba mbili (2) za walimu (2 in 1) katika shule ya sekondari Bupigi zinazojengwa kupitia mradi wa SEQUIP na kwamba mradi huo upo hatua za ukamilishaji.

Lakini pia mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme amekagua ujenzi wa shule mpya ya msingi ya Jitegemee (Nguzombili) iliyopo  kata ya Maganzo ambapo ujenzi huo unatekelezwa kupitia mradi wa BOOST.

Kwa upande wake mkuu wa Wilaya ya Kishapu Mhe. Joseph Mondest Mkude amesema Wilaya hiyo kupitia serikali itaendelea kutatua changamoto zilizopo ili kuondoa usumbufu kwa wananchi.

Ameeleza kuwa katika miradi inayotekelezwa Wilaya ya Kishapu inaendelea kusimamia upatikanaji wa mafundi waaminifu katika utekelezaji wa miradi hiyo ambapo amesema wanaendelea kushirikiana na wadau wote wa maendeleo katika kusimamia na kufuatilia utekelezaji wa miradi.

DC Mkunde ametumia nafasi hiyo kumshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kutoa fedha kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo.

“Kwa niaba ya wananchi wa Wilaya ya Kishapu nachukua fursa hii kuishukuru Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa juhudi anazoendelea nazo za kutafuta fedha kwa ajili ya kujenga miradi ya Maendeleo (Maji Mijini na Vijijini, Ujenzi wa vituo vya Afya, Barabara, Vyumba vya madarasa kwa shule za Msingi na Sekondari na miradi mikubwa ya kimkakati”.

“Watumishi wote Tunamuahidi kuwa tupo pamoja nae katika kusimamia miradi ya maendeleo na kuakisi utendaji wake wa kazi uliotukuka”.amesema DC Mkude

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme leo Jumatatu Oktoba 30,2023 amefanya ziara ya siku moja kutembelea na kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo katika Wilaya ya Kishapu akiwa ameambatana na viongozi mbalimbali akiwemo kamanda wa jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga kamishna msaidizi wa Polisi Janeth Magomi.

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Solomon Mndeme akiwa ameongozana na viongozi mbalimbali katika zoezi la kutembelea ujenzi wa nyumba  mpya  ya mkuu wa Wilaya ya Kishapu Jumatatu Oktoba 30,2023.


Wananchi wa Ngundangali, Dugushilu, Kakola, Seseko na Mpumbula 

Wananchi wa Ngundangali, Dugushilu, Kakola, Seseko na Mpumbula 

This is received, thanks for your comments, will come back to you

Previous Post Next Post