MAHAFARI YA 14 SHULE YA SEKONDARI IDAHINA USHETU, WAIOMBA SERIKALI NA WADAU KUSHUGHULIKIA CHANGAMOTO ZILIZOPO


Na Mapuli Misalaba, Shinyanga

Jumla ya wanafunzi 109 kati yao wavulana 57, wasichana 52 wamehitimu kidato cha nne mwaka huu 2023 katika shule ya sekondari Idahina iliyopo Halmashauri ya Wilaya ya Ushetu Mkoani Shinyanga.

Shule hiyo imefanya mahafari ya 14 ya wanafunzi  kuhitimu kidato cha nne tangu kuanzishwa kwake Mwaka 2007.

Mahafari hayo yamehudhuriwa na viongozi mbalimbali wa serikali pamoja na viongozi wa chama cha mapinduzi CCM kata ya Idahina akiwemo Diwani wa kata hiyo Mhe. Mathias Makashi.

Katika risala ya wahitimu iliyosomwa na Elen Reuben Petro imebainisha mambo mbalimbali ikiwemo mafanikio na changamoto huku wakiiomba serikali, wadau, jamii kwa kushirikiana na wazazi kuendelea kutatua changamoto zinazoikabili shule hiyo.

Changamoto hizo ni pamoja na ukosefu wa umeme hali inayotanjwa kuathiri afya ya macho kwa wanafunzi, changamoto ya bomba la maji katika Bweni la wasichana pamoja na changamoto ya ukosefu wa walimu wa kike.

“Suala la umeme linaathiri Afya ya macho hasa wakati wa usiku ambapo wanafunzi wengi tunahangaika kwa kutumia mwanga hafifu wa umeme  wa jua wengi tunapata changamoto ya macho hasa nyakati za masika”.

“Shule ya  sekondari Idahina inakabiliwa na changamoto ya bomba la maji kwenye Bweni la wasichana ambapo linahitajika kukamilishwa maana wananchi maana wananchi na wazazi wetu tuliwashuhudia wakisomba mawe, mchanga, kokoto na kuchangia fedha kwa ajili ya ujenzi wa Hostel kwa wasichana tunaomba utusaidie kukamilisha Bweni hilo ili kuondoa changamoto ya kubanana kwa wasichana katika Bweni moja”.amesema Elen

“Changamoto ya kukosa walimu wa kike ambao ni msaada mkubwa wa kusikiliza, kushauri na kutatua changamoto za watoto wa kike hapa shuleni tunaomba utusaidie kupata walimu wa kike hata wawili”.

“Lakini pia kwa miaka minne yapo mafanikio katika shule hii ulifanyika ujenzi wa vyoo vya kisasa, ujenzi wa nyumba 14 vya kisasa, ununuzi wa mashine ya kuchapisha mitihani, ununuzi wa mashine ya kusaga unga pamoja na uchangiaji mzuri wa chakula shuleni”.amesema Elen

Akizungumza mgeni rasmi Bwana Julius lugobi kwa niamba ya mbunge wa jimbo la Ushetu ataendelea kushirikiana katika kutatua changamoto zinazoikabili  shule ya sekondari Idahina ili wanafunzi waweze kusoma katika mazingira mazuri na salama.

Kwa upande wake Diwani wa kata ya Idahina Mhe. Mathias Makashi amewapongeza wanafunzi hao kwa kuhitimu kidato cha nne huku akiwasihi kutokata tamaa ili waweze kufikia ndoto zao  ambapo pia amewaomba wazazi kutimiza wajibu  kwa watoto wao na kuhakikisha wanasoma ili kuwa na Taifa la vijana wasomi.

 

Wahitimu wa kidato cha nne Mwaka huu 2023 katika shule ya sekondari Idahina wakiingia ukumbini.


This is received, thanks for your comments, will come back to you

Previous Post Next Post