TARURA JIANDAENI KUBORESHA MIUNDOMBINU YA BARABARA KABLA YA MVUA ZA EL NINO

2.Pichani kuanzia kushoto ni Afisa Rasilimali watu wa Wakala huo Mkoa wa Arusha Lissa Mziray, Kaimu Meneja wa Tarura Mkoa wa Arusha Mhandisi Albert Kyando na Meneja wa Tarura wilaya ya Karatu Mhandisi Msetu Madara wakifuatilia hotuba ya DC.Kolimba
1.Mkuu wa Wilaya ya Karatu Dadi Kolimba akiongea wakati akifungua Kikao Kazi cha Watumishi wa Wakala wa barabara za vijijini na mijini Tarura kinachofanyika Mjini Karatu

Sehemu ya watumishi wa Wakala wa barabara za vijijini na mijini Tarura Mkoa wa Arusha wakifuatilia hotuba ya Mkuu wa Wilaya ya Karatu Dadi Kolimba katika kikao Kazi cha Tarura Mjini Karatu

 Na Ahmed Mahmoud


Mkuu wa Wilaya ya Karatu Dadi Kolimba amewataka watumishi wa Tarura Mkoa wa Arusha kutatua changamoto za Miundombinu kabla ya mvua za El nino kuanza.

Ameyasema hayo wakati akifungua kikao Kazi cha Watumishi wa Wakala wa barabara za vijijini na mijini Tarura Mkoa wa Arusha ikinachofanyika kwa siku mbili wilayani Karatu Mkoa wa Arusha ambapo amesema taarifa za Mamlaka ya hali ya hewa nchini kuwepo kwa mvua hizo tujipange sawia kutatua changamoto kabla na baada ya mvua hizo.

Amesema kwamba Kuna shughuli ambazo zinatakiwa kufanyika kabla ya maafa lakini kunashughuli zinatakiwa kufanyika wakati wa maafa na Kuna shughuli ambazo zinatakiwa kufanyika baada ya maafa na sekta yenu ni muhimu sana Sasa tukahakikishe katika ile mipango yetu tunaisimamia vizuri.

"Maeneo ambayo yamekuwa na changamoto mkayaweke vizuri kwa kuzibua mitaro kuweka makaravati kabla ya athari Kubwa haijatokea kwa kuhakikisha tunaisimamia vizuri ili mvua zinapokuja tusiwe na madhara makubwa"

Aidha sisi wote humu tunalo jukumu Kubwa la kuhakikisha barabara zote za vijijini na mijini zimekaa vizuri ili kusaidia kusitokee maafa makubwa kupitia kamati za wataalamu kuanzia ngazi za kata wilaya hadi Mkoa ,lakini pia tujiandae endapo yatatokea maafa kuhakikisha tunatumia vizuri Elimu zetu kuokoa kusije kukatokea maafa makubwa.

Kwa mujibu wa Kolimba Moja ya malengo yenu ni kujadili mipango ya huko mbeleni kwa sababu ya Utalii mjaribu kuimarisha miundo mbinu ya barabara zetu hapa mjini.

Wakati Mimi naingia hapa 2021 tulipata bajeti ya million 928 lakini kwa mwaka wa fedha 2022/23 tumeanza kupata bajeti ya billion 2.3 ambapo wilaya ya Karatu Ina mtandao wa barabara kilometa 712 wakati naingia tulikuwa na barabara za lami km 0.6 Sasa tuna km 2.8.

Alisema kwa ushirikiano huo wataenda mbali zaidi kuimarisha barabara zetu lakini barabara ambazo zimetengenezwa kwa kiwango cha changarawe nikaribia km 166 hivyo tunampongeza Mh. Rais Samia Suluhu Hassan kwa fedha nyingi zinazoletwa katika wilaya yetu na Kazi Kubwa inafanyika.

Kaimu Meneja wa Tarura Mkoa wa Arusha Mhandisi Albart Kyando amesema wamepokea maelekezo ya Mkuu wa Wilaya na wameshaanza kuchukuwa tahadhari zote kwa kuandaa Mpango mkakati kama taasisi wa kukabiliana na maafa ambao umefuata Muongozo uliotolewa na kamati ya maafa.

Hata hivyo kwa Sasa tunakazi zilizofanyika tumepokea tahadhari tokea mwezi wa 7 na Kazi ya kwanza ilikuwa ni Madaraja na vivuko vyote pale penye changamoto tumeshaanza kuchukuwa hatua kwa kutenga baadhi ya rasilimali ambazo tulikuwa tutumie katika Kazi za kawaida tumeelekeza huko hivyo itakapotokea tutaendelea kukabiliana ili kupunguza athari.

"Mara nyingi bajeti zetu tumekuwa tunapanga kulingana na kufungua barabara mpya kutokana na vyanzo vya mfuko wa Jimbo na tozo kwa kipaumbele cha kwanza kuwa maeneo ya uzalishaji kwa kuongeza nguvu hivyo ni lazima tuwe na vipaumbele vya ujenzi ili kuondoa migogoro tumekuwa tukitoa Elimu kwa wananchi na madiwani "

This is received, thanks for your comments, will come back to you

Previous Post Next Post