MSTAHIKI MEYA MASUMBUKO AELEKEZA MATANGAZO YA ZABUNI KUWEKWA WAZI

Na Moshi Ndugulile

Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga Elius Ramadhan Masumbuko  kwa kushirikiana na serikali kuu imeendelea kubaini maeneo yenye uhitaji wa kujengwa Shule za Msingi na sekondari, kama hatua ya kuondoa changamoto ya wanafunzi kutembea umbali mrefu kufuata masomo

Hayo yameelezwa na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga Mwalimu Alexius kagunze,kwenye kikao cha Baraza la madiwani ,wakati akijibu swali lililoulizwa na Diwani wa kata ya koladoto Mheshimiwa Mussa Elias aliyetaka kujua mkakati wa serikali kujenga shule katika kijiji cha Galamba ili kuondoa changamoto ya wanafunzi kutembea umbali mrefu

Kagunze amesema ili kuondoa changamoto hiyo serikali imeendelea kutoa fedha kwa ajili ya utekelezaji wa miradi mbali mbali ikihusisha sekta ya Elimu

Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga kwa kushirikiana na serikali kuu imeendelea kubaini maeneo yenye uhitaji wa kujengwa Shule za Msingi na sekondari, kama hatua ya kuondoa changamoto ya wanafunzi kutembea umbali mrefu kufuata masomo

Hayo yameelezwa na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga Mwalimu Alexius kagunze,kwenye kikao cha Baraza la madiwani ,wakati akijibu swali lililoulizwa na Diwani wa kata ya koladoto Mheshimiwa Mussa Elias aliyetaka kujua mkakati wa serikali kujenga shule katika kijiji cha Galamba ili kuondoa changamoto ya wanafunzi kutembea umbali mrefu

Kagunze amesema ili kuondoa changamoto hiyo serikali imeendelea kutoa fedha kwa ajili ya utekelezaji wa miradi mbali mbali ikihusisha sekta ya Elimu

matangazo ya zabuni  zote, ili kutoa nafasi  kwa Wananchi wote kutumia fursa hizo

Ametoa maelekezo hayo jana kwenye kikao cha baraza la Madiwani wa Halmahauri ya Manispaa ya Shinyanga,kilichofanyika kwenye ukumbi wa Lews kalinjuna Mjini Shinyanga

Meya huyo amesisitiza kuwa matangazo yote ya zabuni yawekwe wazi kwenye maeneo yote ya wazi ikiwemo kubandikwa kwenye mbao za matangazo katika ofisi za maafisa watendaji wa kata, ili wananchi wapate nafasi ya kusoma na kutumia fursa hiyo.

Wakati huo huo Mstahiki Meya amewataka   Madiwani kuendelea kushirikiana na na watumishi wa halmashauri wakiwemo wataalamu na watendaji wengine katika hatua za kusukuma maendeleo na ustawi wa wananchi.

“Lakini katika baadhi ya maeneo watendaji wanataka usirikiano na Madiwani,sasa kuna mahali wanakutana na changamoto za kiutendaji waaoingia kwenye shughuli za uwajibikaji,kwamba wapiga kura wangu waachwe,sasa waache kwa sababu zipi ?naomba tuangalie shughuli za serikali na shughuli zetu kama wawakilishi,tuwape nafasi watendaji wafanye shughuli zao,hapa tumeona kuna miradi mingi ambayo tunasema itekelezwe,nah ii miradi inahitaji mapato,sasa kama tunasema watendaji wasiwaingilie wananchi,kwa sababu ya kigezo cha uchaguzi manake hata hiyo miradi haiwezi kutekelezeka,manake itekelezeke  baada ya Uchaguzi,na sisi mikakati yetu ipo kwenye mpango wa utekelezaji,kwa hiyo naomba tuwape ushirikiano,sasa tusimamie mambo haya,tusiwape wakati mgumu wa kufanya kazi zao,kwani na wao wana wajibu wa kutoa taarifa za utekelezaji kwa mamlaka zinazowatuma”amesema Mstahiki Meya.

Wakati huo huo Mkurugenzi wa Manispaa ya Shinyanga Mwalimu Alexius Kagunze amesema Halmashauri hiyo kwa kushirikiana na serikali kuu imeendelea kubaini maeneo yenye uhitaji wa kujengwa Shule za Msingi na sekondari, kama hatua ya kuondoa changamoto ya wanafunzi kutembea umbali mrefu kufuata masomo

Ametoa kauli hiyo wakati akijibu swali lililoulizwa na Diwani wa kata ya koladoto Mheshimiwa Mussa Elias aliyetaka kujua mkakati wa serikali kujenga shule katika kijiji cha Galamba ili kuondoa changamoto ya wanafunzi kutembea umbali mrefu,

Kagunze amesema ili kuondoa changamoto hiyo serikali imeendelea kutoa fedha kwa ajili ya utekelezaji wa miradi mbali mbali ikihusisha sekta ya Elimu

“Serikali imeendelea kutuma fedha kwa ajili ya shule au miradi mbali mbali ambapo katika eneo hilo walipita wataalamu kutoka katika wizara ofisi ya Rais TAMISEMI na kubainisha maeneo ambayo yalionekana kwamba yatafaa kuongezewa shuleili kupunguza wanafunzi waliojaa katika shule moja lakini kuondoa changamoto ya umbali,na mfano mzuri ni shule ya  Sekondari Ngokolo B, (Siyo jina rasmi)ambayo imeletewa fedha shilingi Milioni 603,lengo ni kupunguza idadi ya wanafunzi.

Mategemeo yetu ni kufanya ufuatiliaji kutoka serikalini ili kuona kama watatupatia fedha kwa sababu eneo lililotajwa wanafunzi wanatoka mbali”ameeleza Mkurugenzi huyo.

Katika kikao hicho cha Baraza la Madiwani,waheshimiwa hao wamewasilisha taarifa za utekelezaji ambapo pamoja na kubainisha mafanikio,wametaja pia changamoto zilizopo katika kata zao.

Akizungumza katika kikao cha Baraza la Madiwani Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi CCM Wilaya ya Shinyanga Mjini Bwana Anold Makombe amepongeza juhudi za Madiwani kwa kushirikiana na Mkurugenzi pamoja na watumishi wa Halmashauri katika utekelezaji wa miradi  hali inayochochea maendeleo na ustawi wa wananchi.

 

Mstahiki meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga (aliyesimama) akizungumza kwenye kikao cha Baraza la madiwani.

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga  Mwalimu Alexius Kagunze akizungumza kwenye kikao cha Baraza la Madiwani .

Kikao cha Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga kikiendeleo katika ukumbi wa Lewis Kalinjuma..


This is received, thanks for your comments, will come back to you

Previous Post Next Post