MKUU WA MKOA WA SHINYANGA MHE. CHRISTINA MNDEME ATEMBELEA UWANJA WA NDEGE IBADAKULI, OFISI YA MWENDESHA MASHTAKA NA HOSPITALI YA RUFAA YA MKOA WA SHINYANGA

Serikali Mkoa wa Shinyanga imesema itaendelea kushughulikia changamoto zilizopo katika Hospitali ya rufaa ya Mkoa wa Shinyanga ikiwemo ujenzi wa majengo mapya pamoja na uboreshaji wa miundombinu ya barabara ili kuepusha usumbufu uliopo.

Hayo yamebainishwa na Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Bi. Christina Mndeme baada ya kupokea changamoto katika taarifa fupi iliyosomwa na mganga mfawidhi wa Hospitali ya rufaa ya Mkoa wa Shinyanga iliyopo Mwawaza Dkt. Luzila John leo Jumanne Oktoba 31, 2023.

Dkt. Luzila ametaja baadhi ya changamoto zinazoikabili Hospitali ya rufaa ya Mkoa wa Shinyanga ikiwemo upungufu wa watumishi, ukosefu wa Mochwari pamoja na ubovu wa miundombinu ya barabara inayotoka mjini kuendelea katika Hospitali hiyo ya rufaa.

“Tunachangamoto ya uchache wa majengo  Maabala imepelekwa ambako siyo sehemu yake kwahiyo wagonjwa wanapata wakati mgumu kwa ajili ya ubali wa majengo haya, upungufu wa watumishi tunaupungufu wa asilimia 47, changamoto nyingine ni kuharibika kwa barabara ambayo haijajengwa kwa kiwango cha lami imekuwa ni usumbufu mkubwa kwa wagonjwa na watumishi gali zinaharibika mara kwa mara kwa sababu ya ubovu wa barabara tunakuomba kama ikiwezekana jambo hili liharakishwe ili kupunguza usumbufu kwa wananchi wa Mkoa wa Shinyanga” amesema Dkt. Luzila

“Tunaishukuru sana serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kutoa fedha kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu, ununuzi wa vifaa tiba pamoja na kutuletea watumishi”.

Dkt. Luzila amesema Hospitali ya rufaa ya Mkoa wa Shinyanga inatoa huduma za kimatibabu kwa asilimia mia moja pamoja na huduma za matibabu ya wagonjwa wa ndani na wa nje zinafanyika ikiwemo huduma za kliniki za kibingwa za magonjwa ya ndani upasuaji wa watoto pamoja na magonjwa ya akina mama kwa siku zote za wiki.

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme amesema kipaumbele cha serikali ya Mkoa wa Shinyanga ni kuitengeneza barabara inayotoka Mwawaza hadi kata ya Ndala kwa kiwango cha lami ili kuondoa usumbufu wa wagonjwa na wakazi wa Mkoa wa Shinyanga.

“Barabara hii ambayo ni kilometa tatu kutoka Ndala kuja Mwawaza ni changamoto ambayo tunaishughulikia napenda kuahidi kwamba barabara hii tunakwenda kuitengeneza kwa kiwango cha lami malengo tufike mpaka kijijini Mwawaza lakini tunaanza kwanza kuishia hapa Hospitali ya rufaa na tutaanza na mitalo hicho ni kipaumbele cha serikali ya Mkoa kuhakikisha kwanza fedha tutakayoipata ni kujenga hizi kilometa tatu haziwezi kutushinda kwahiyo suala hili tunalishughulikia ili tuondoe changamoto iliyopo ya ubuvu wa barabara”.amesema  RC Mndeme.

Mhe. Mndeme amewataka watumishi wa Hospitali hiyo ya rufaa ya Mkoa wa Shinyanga kuendelea kutoa elimu ya afya kwa wananchi ili kuepukana na athari mbalimbali ikiwemo magonjwa yasiyoambukiza, magonjwa ya kisukari pamoja na magonjwa na shinikizo la damu.

Amewasisitiza watumishi hayo kufanyakazi kwa kuzingatia sheria, taratibu na maelekezo ya wizara hiyo ambapo  amemuagiza mganga mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Dkt. Yudas Ndungile, mganga mfawidhi Dkt. Luzila John pamoja na wakuu wa idara kusimamia upotevu na wizi wa dawa na vifaa tiba.

RC Mndeme amewapongeza watumishi wa Hospitali hiyo ya rufaa ya Mkoa wa Shinyanga huku akiwakumbusha kuendelea kutumia lugha nzuri na kuepuka kuongea na simu au kuchezea simu wakati wa kumhudumia mgonjwa.

Aidha mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme katika ziara yake leo ametembelea ujenzi wa ofisi ya mwendesha mashtaka Mkoa wa Shinyanga ambapo thamani ya mradi huo ni zaidi ya shilingi Bilioni mbili mradi na kwamba umefikia asilimia 60 ya ujenzi na  unatarajiwa kukamilika Disemba 28,2023.

Mkuu wa Mkoa huyo pia ametembelea ujenzi wa kiwanja cha ndege katika kata ya Ibadakuli Manispaa ya Shinyanga huku akiagiza ukamilike kwa wakati ili uanze kutumia na kufikia malengo yaliyokusudiwa na serikali.

Awali akisoma taarifa fupi ya utekelezaji wa upanuzi wa kiwanja cha ndege  Mkoa wa Shinyanga, meneja TANROADS Mkoa wa Shinyanga Mhandisi Mibara Ndirimbi amesema ujenzi wa kiwanja hicho umefikia asilimia 4.5 mpaka sasa.

“Muda wa mkataba ni miezi 18 tarehe ya kumaliza mradi huu ni Novemba 20,2024 mkandarasi yupo eneo la mradi na hatua za utekelezaji wa kazi unaendeleo ukiwa umefikia asilimia 4.5, ujenzi wa kiwanja hiki cha ndege utawapunguzia ada wananchi wa Mkoa wa Shinyanga na Mikoa jirani tunatarajia uwepo wa kiwanja hiki utafungua fursa za uwekezaji katika Mkoa wetu wa Shinyanga napenda kukuhakikishia kuwa matarajio yetu mkandarasi atamaliza kazi ndani ya muda uliopangwa”.amesema Mhandisi Ndirimbi

Kwa upande wake meneja miradi wa kampuni ya CHICO Shi Yinlei na mhandisi mkazi wa mradi huo Nasser Elgohary  wamesema mradi huo utakamilika kwa wakati huku wakiahidi kutoa kipaumbele kwa wakazi wa Mkoa wa Shinyanga katika suala la ajira.

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme ameendelea na ziara zake ambapo leo ametembelea na kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo katika Manispaa ya Shinyanga ziara hiyo imehudhuriwa na viongozi mbalimbali wa serikali akiwemo kamanda wa jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga kamishna msaidizi wa Polisi Janeth Magomi pamoja na mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Johari Samizi.

 

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme akisalimiana na viongozi mbalimbali leo Oktoba 31,2023 baada ya kuwasili katika eneo la uwanja wa ndege wa Mkoa wa Shinyanga unaojengwa kata ya Ibadakuli. 

This is received, thanks for your comments, will come back to you

Previous Post Next Post