Naibu Waziri wa Mali asili na utalii ataka ushirikiano wa nchi na nchi kudhibiti biashara haramu ya Wanyamapori

 Na Queen  Lema, Arusha

TAASISI mbalimbali ambazo zinasimamia na kudhibiti biashara haramu za wanyama pori zimetakiwa kuongeza umoja pamoja na ushirikiano ili kudhibiti wimbi la biashara haramu ya wanyamapori ambayo inaendelea kwenye baadhi ya nchi. 

Aidha biashara hiyo inaelezwa kuwa imekuwa ikisababisha madhara mbalimbali kama vile ukosefu wa kodi, ushuru, na hata usalama wa wanyama kwa kuwa hata njia ambazo zinatumika huwa ni njia za kujificha 

Hayo yameelezwa na Naibu waziri wa Mali asili na Utalii, Dunstan Mgandulwa wakati akifungua mafunzo ya kikanda juu ya kukabiliana na usafirishaji haramu wa wanyamapori kati ya Afrika na Asia. 


Waziri huyo alisema kuwa nchi za Afrika na Asia zimefanikiwa kubarikiwa kuwa na maliasili pamoja na wanyamapori ambao ni vivutio.

Alisema kuwa pamoja na kuwa nchi zimebarikiwa lakini bado kuna genge kubwa la baadhi ya wananchi au raia kutoka nchi jirani kufanya biashara haramu za wanyama hasa kwa kupitia mipaka baina ya nchi na nchi.

"Haya mafunzo ni muhimu sana kwa maendeleo ya nchi na nchi lakini pia kuhakikisha kuwa jitihada na makubaliano ambayo yalifanyika kule Lusaka yafuatwe, ili yaweze kufanikiwa kunaitajika ushirikiano mipakani ikiwa ni pamoja na kuondoa vikwazo baina ya nchi na nchi"aliongeza.

Akiongelea hali ya biashara haramu kwa Tanzania alisema kuwa hali hiyo imepungua kwa kiwango kikubwa sana  tofauti na hapo awali ambapo biashara haramu  ya wanyama pori ilishamiri. 

"Tanzania imepiga hatua kubwa sana hasa kwenye biashara haramu lakini hata usafirishaji haramu wa wanyama ambao ni rasilimali za Taifa bado tunaendelea kupigania maslahi ya taifa kwa kuwa biashara haramu inachangia kwa kiwango kikubwa kushusha hata maslai ya taifa"aliongeza


Akiongea kwa niaba ya washiriki wa mafunzo hayo Wakili Salimu Msemo alisema kuwa mafunzo hayo ambayo yameshirikisha nchi mbalimbali yataweza kuwasaidia endapo kama kutakuwepo na umoja baina ya nchi na nchi,mipaka na mipaka, sanjari na kuwepo kwa mbinu za upelelezi ambazo zitaweza kuwanasa wahalifu kwa haraka.

This is received, thanks for your comments, will come back to you

Previous Post Next Post