RC MNDEME AWAOMBA AKINA MAMA KUSIMAMIA SUALA LA LISHE NA UKATILI KWA WATOTO, CHANGAMOTO YA UMEME KUISHA MKOANI SHINYANGA

Na Mapuli Misalaba, Shinyanga

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme amewaomba akina mama Mkoa wa Shinyanga kusimamia vyema suala la lishe kwa watoto ili kumaliza tatizo la udumavu.

Ameyasema hayo wakati akizungumza na jumuiya ya wanawake wa kiislam Mkoa wa Shinyanga (JUWAKITA) ambapo pamoja na mambo mengine amesema Mkoa wa Shinyanga mpaka sasa una asilimia 27.5 ya tatizo la udumavu.

Rc Mndeme amewaomba akina mama kuwa  mstari wa mbele kusimamia suala la upatikanaji wa lishe bora kwa watoto ili kuondoa tatizo la udumavu kwa watoto.

“Akina mama sisi ni wajibu wetu kusimamia kuhakikisha kwamba watoto wetu hasa walio na umri chini ya miaka mitano wanapata lishe bora na tuondokane kabisa kutoka asilimia 27.5 tufike asilimia 0 linawezekana mtoto chini ya miaka mitano ale chakula ambacho kinafaa tuondokane na kuwalisha watoto chakula kwa mazoea kwa sababu sisi akina mama ni wasimamizi wakubwa wa makuzi katika familia zetu tusimamie suala la lishe kwa watoto wetu ili udumavu ndani ya Mkoa wetu uondoke bahati nzuri Mkoa wetu una kila aina ya chakula hatuna sababu ya kuendelea kuwa na udumavu katika Mkoa wa Shinyanga akina mama wenzagu naomba tumuunge mkono Rais wetu Dkt. Samia Suluhu Hassan masuala ya lishe tuyasimamie”.amesema RC Mndeme

RC Mndeme amewaomba wanawake katika Mkoa wa Shinyanga kuendelea kukemea mmomonyoko wa maadili ikiwa ni pamoja na kutokomeza ukatili unaoendelea kufanyika kwenye familia ikiwemo vitendo vya ubakaji na ulawiti.

“Tukemee suala la mmomonyoko wa maadili miongoni mwa jamii yetu tukemee vitendo vya ubakaji na ulawiti lakini tuna kila sababu ya kuyaongea haya kuanzia ngazi ya familia, tuongee na familia zetu utandawazi unakua tuyaige yale mazuri yasiyofaa tuachane nayo lakini tumwambie mtoto kwamba hilo eneo ni eneo lako hakuna mtu mwingine mwenye ruhusa ya kupashika tuendelee kuwafunda watoto wetu kuanzia wakiwa watoto mpaka wakubwa wakatae ukatili lakini tuwaambie watoto wetu wasitamani utajiri wa haraka haraka Nyumba Gari tafuta kipato kilicho halali haya matendo ya ubakaji ulawiti ni chukizo mbele za mwenyezi Mungu”.amesema RC Mndeme

Katika hatua nyingine RC Mndeme ameelezea mafanikio yaliyopatikana katika kipindi cha Rais wa awamu ya sita Dkt. Samia Suluhu Hassan ambapo amesema kwa muda mfupi Rais Dkt. Samia ameleta fedha takribani tirioni moja kwa ajili ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo katika sekta mbalimbali ikiwemo Elimu, Afya pamoja na miundombinu Mkoani Shinyanga.

Aidha Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme ameeleza kuwa Rais Dkt. Samia tayari ametoa fedha zaidi ya Bilioni 275 ambazo zitatekeleza mradi wa kuzalisha umeme kwa njia ya jua katika Wilaya ya Kishapu ambapo amesema hatua hiyo itasaidia kumaliza tatizo la kukatika kwa umeme Mkoani Shinyanga.

Baadhi ya viongozi wa jumuiya wa wanawake wa kiislam Mkoa wa Shinyanga (JUWAKITA) waliohudhuria hafla hiyo wamesema wataendelea kushirikiana na serikali ikiwemo kupambana na ukatili na uhalifu ambao unachangia kurudisha  nyuma maendeleo ya Mkoa wa Shinyanga.

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme amekutana na kuzungumza na wanawake wa jumuiya ya kiislam Mkoa wa Shinyanga ambapo pamoja na mambo mengine wamejadili kuhusu maendeleo huku akipokea changamoto zilizopo Mkoani Shinyanga na kwamba ameahidi kuchukua hatua kwa watu wanaokwenda kinyume na taratibu za Nchi.

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme akizungumza katika hafla hiyo ambayo amekutana na jumuiya ya wanawake wa kiislam Mkoa wa Shinyanga (JUWAKITA) kuzungumzia maendeleo ya Mkoa huo.

Mwenyekiti wa jumuiya ya wanawake wa kiislamu Mkoa wa Shinyanga (JUWAKITA)  Bi. Aisha Juma akizungumza kwenye hafla hiyo.




This is received, thanks for your comments, will come back to you

Previous Post Next Post