SMAUJATA MKOA WA SHINYANGA YAWAKUMBUSHA VIONGOZI NA WADAU WA KUPINGA UKATILI KUKEMEA RUSHWA

Na Mapuli Misalaba, Shinyanga

Mwenyekiti wa kampeni ya shujaa wa maendeleo na ustawi wa jamii Tanzania (SMAUJATA) Mkoa wa Shinyanga Bi. Nabila Kisendi amewakumbusha viongozi pamoja na wadau mbalimbali wa kupinga ukatili kuendelea kukemea rushwa katika utekelezaji wa majukumu yao.

Ameyasema hayo wakati akizungumza na viongozi wa SMAUJATA Wilaya ya Shinyanga vijijini ambapo amesisitiza viongozi hayo kutojihusisha na  rushwa katika utetezi wa haki za wahanga wa ukatili na uhalifu unaoendelea kufanyika kwenye jamii.

Mwenyekiti huyu Nabila Kisendi pamoja na mambo mengine amewahimiza viongozi wa SMAUJATA kuwa mabalozi wazuri wa kupambana na ukatili huku akiwasisitiza kupambana na rushwa ili hatua za kisheria ziendelee kuchukuliwa dhidi ya wahalifu.

Mwenyekiti idara ya maadili SMAUJATA Mkoa wa Shinyanga Bwana Solomon Najulwa (Cheupe) amesema ni muhimu viongozi kuwa waadilifu katika kupambana na rushwa.

Kwa upande wake katibu wa SMAUJATA Mkoa wa Shinyanga Bwana Daniel Kapaya ameiomba serikali kupitia mamlaka husika kuendelea kuchukua hatua kali kwa watu wanaobainika kujihusisha na rushwa ili kutokomeza vitendo hivyo.

Baadhi ya viongozi Wilaya ya Shinyanga vijijini wameahidi kufanya kazi kwa kuzingatia sheria na taratibu zilizopo ili kufikia malengo yaliyokusudiwa na serikali katika kupambana na ukatili.

SMAUJATA Mkoa wa Shinyanga imefanya ziara ya siku moja Wilaya ya Shinyanga vijijini kwa lengo la kuimarisha viongozi ngazi ya Wilaya.

Mwenyekiti wa kampeni ya shujaa wa maendeleo na ustawi wa jamii Tanzania (SMAUJATA) Mkoa wa Shinyanga Bi. Nabila Kisendi akiwasihi viongozi kuepuka rushwa katika utekelezaji wa majukumu yao.

Mwenyekiti wa kampeni ya shujaa wa maendeleo na ustawi wa jamii Tanzania (SMAUJATA) Mkoa wa Shinyanga Bi. Nabila Kisendi akiwasihi viongozi kuepuka rushwa katika utekelezaji wa majukumu yao.

Katibu wa kampeni ya shujaa wa maendeleo na ustawi wa jamii Tanzania (SMAUJATA) Mkoa wa Shinyanga Bwana Daniel Kapaya akizungumza kwenye kikao hicho.

Mwenyekiti idara ya maadili SMAUJATA Mkoa wa Shinyanga Bwana Solomon Najulwa (Cheupe) akizungumza kwenye kikao hicho.

Mwenyekiti idara ya Michezo  SMAUJATA Mkoa wa Shinyanga ambaye pia ni Polisi wa kata ya Ndala afande Alkwin Willa akizungumza kwenye kikao hicho.

Mwenyekiti wa SMAUJATA Manispaa ya Shinyanga Stella Gershom akizungumza kwenye kikao hicho.

Katibu wa SMAUJATA Manispaa ya Shinyanga Hasna Maige akizungumza kwenye kikao hicho.

Mwenyekiti wa SMAUJATA Wilaya ya Shinyanga vijijini Bwana Emmanuel Makolo akizungumza kwenye kikao hicho.

Kikao cha viongozi wa SMAUJATA ngazi ya Mkoa pamoja na viongozi ngazi ya Wilaya ya Shinyanga vijijini kikiendelea.

Mwenyekiti wa kampeni ya shujaa wa maendeleo na ustawi wa jamii Tanzania (SMAUJATA) Mkoa wa Shinyanga Bi. Nabila Kisendi akiwa kwenye picha ya pamoja na viongozi mbalimbali.

Mwenyekiti wa kampeni ya shujaa wa maendeleo na ustawi wa jamii Tanzania (SMAUJATA) Mkoa wa Shinyanga Bi. Nabila Kisendi akiwa kwenye picha ya pamoja na viongozi mbalimbali.

This is received, thanks for your comments, will come back to you

Previous Post Next Post