AJALI YA MOTO KATIKA MTAA WA MWASELE B KATA YA KAMBAREGE MANISPAA YA SHINYANGA

Kamanda wa Jeshi la Zimamoto na uokoaji Mkoa wa Shinyanga Mrakibu Martin Nyambala ametoa wito kwa wazazi na walezi kuwajibikia suala la ulinzi na usimamizi kwa watoto wanapokuwa nyumbani ili kuepukana na majanga mbalimbali yanayoweza kujitokeza ikiwemo ajali za moto.

Ametoa wito huo  wakati akizungumza kufuatia ajali ya moto iliyotokea Oktoba 20,2023 majira ya saa sita mchana katika Mtaa wa Mwasele B Kata ya Kambarege Manispaa ya Shinyanga na kuteketeza nyumba ya Bwana Rojaz Pius.

Kamanda huyo amesema taarifa za awali zimeonesha kuwa moto huo umesababishwa na mtoto aliyekuwa akicheza ndani ya nyumba hiyo lakini Jeshi hilo linaendelea na uchunguzi ili kubaini ukweli wa chanzo cha tukio hilo.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Mtaa huo Bwana Cosmas Lukas ameeleza namna alivyopokea taarifa za tukio hilo na hatua mbalimbali zilizochukuliwa kunusuru mali na wakazi wa familia hiyo.

Nao baadhi ya majirani walioshuhudia tukio hilo wamepongeza hatua mbalimbali zilizochukuliwa na wananchi kwa kushirikliana na Jeshi la Zimamoto na uokoaji pamoja na Shirika la Umeme Tanzania TANESCO kudhibiti moto huo.

This is received, thanks for your comments, will come back to you

Previous Post Next Post