WANAWAKE WA MKOA WA SHINYANGA WAMPONGEZA RAIS SAMIA KWA KUTOA FEDHA NYINGI ZA UTEKELEZAJI WA MIRADI YA MAENDELEO.

Na Mapuli Misalaba, Shinyanga

Wanawake  Mkoa wa Shinyanga wameipongeza serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kutoa fedha kwa ajili ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwemo sekta ya elimu, afya, maji na miundombinu ya barabara katika Halmashauri zote za Mkoa wa Shinyanga.

Wametoa pongezi hizo leo Alhamis Oktoba 12,2023 kwenye kongamano la wanawake wa Mkoa wa Shinyanga ambalo limeratibiwa na Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme kwa lengo la kumshukuru na kumpongeza Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kutoa fedha za miradi ya maendeleo ili kutatua changamoto zinazowakabili wakazi wa Mkoa wa Shinyanga na kuchochea uchumi mkoani humo.

Kongamano hilo limefanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa Savannah shule ya kimataifa na kuhudhuriwa na wanawake mbalimbali kutoka katika Wilaya zote za Mkoa wa Shinyanga ,wakiwemo wajasiliamali,wanasiasa,wakulima,watumishi wa serikali makampuni,mashirika na taasisi binafsi.

 Katika taarifa  yake aliyoitoa leo kwenye kongamano la wanawake wa Mkoa wa Shinyanga, Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme amesema  serikali chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan imeendelea kuwekeza kwenye  sekta zote hivyo kuchochea Maendeleo ya kiuchumi na kijamii katika upatikanaji wa huduma bora za kijamii

RC Mndeme amesema serikali imeendelea kuboresha huduma za kijamii katika sekta mbalimbali ikiwemo Elimu,Afya,Maji, kilimo,viwanda na uwekezaji pamoja na Miundombinu.

Amesema Mkoa wa Shinyanga umepokea fedha takribani shilingi tirioni moja kwa ajili ya matumizi ya kawaida na miradi ya maendeleo katika sekta mbalimbali ikiwemo sekta ya elimu, afya na miundombinu ya barabara.

Ameeleza kuwa ilani ya chama cha mapinduzi 2020/2025 imeendelea kutekelezwa kwa uwazi ,umahili na mafanikio ikiwemo makusanyo ya maduhuri na mapato ya serikali.

"Wanawake wa Mkoa wa Shinyanga tumeamua kumpongeza Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa sababu Shinyanga ya sasa siyo Shinyanga ya zamani maendeleo makubwa tunayashuhudia ya kiuchumi naya kijamii sisi wanashinyanga tunasema kila kijiji kimefikiwa kazi inaendelea kwa vitendo".

"Baadhi ya mafanikio ambayo tumeyapata wanashinyanga na tunaendelea kuyapata kupitia uongozi thabiti wa Dkt. Samia Suluhu Hassan makusanyo ya maduhuri na mapato ya serikali, ukusanyaji wa mapato ya ndani ya Halmashauri za Mkoa wa Shinyanga umeongezeka kutoka shilingi Bilioni 22 na Milioni 349 na laki nane na sita kwa Mwaka 2021/2022 na sasa tumefikia makusanyo ya shilingi Bilioni 31 na milioni 263 na 41 elfu kwa Mwaka 2022/2023 kupitia uongozi thabiti wa Mhe. Rais Samia makusanyo ya Halm ashauri yameongezeka kwa asilimia 41".

"Ongezeko hili linamalisha kuwa upelekeaji na uboreshaji wa huduma kwa wananchi umeongezeka kwa asilimia 41 zikiwemo ujenzi wa Hospitali, vituo vya afya, zahanati, madarasa, matundu ya vyoo, mabweni, masoko, nyumba za watumishi, usafi wa mazingira, uboreshaji wa bustani za mji na kadharika".amesema RC Mndeme

Amebainisha kuwa serikali imetoa shilingi bilioni 386 kwa shirika la usambazaji umeme  TANESCO Mkoa wa Shinyanga kwa ajili ya mradi wa kusambaza umeme vijijini ikiwa ni kwa awamu ya tatu mzunguko wa pili kwa vijiji 240 kwa shilingi bilioni 60.8 kwa wilaya zote tatu

Aidha katika Kongamano hilo mada ya kulinda maadili kwa jamii hasa watoto ni kati ya mada zilizowasilishwa  kwa washiriki wa kongamano la wanawake wa Mkoa wa Shinyanga.

Kupitia kongamano hilo wanawake pia wamekumbushwa kuchangamkia fursa zote zinazojitokeza mbele yao ikiwemo  mikopo inayotolewa na Halmashauri,taasisisi za kifedha ili waweze kujikomboa  kiuchumi.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme akizungumza kwenye kongamano la wanawake wa Mkoa wa Shinyanga lenye lengo la kumpongeza Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kutoa fedha kwa ajili ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo.







This is received, thanks for your comments, will come back to you

Previous Post Next Post