JESHI LA POLISI MKOA WA SHINYANGA LAENDELEA NA MISAKO KUBAINI WAHALIFU, VITU NA VIELELEZO MBALIMBALI VYA KAMATWA

Na Mapuli Misalaba, Shinyanga

Jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga limeendelea na misako ambapo katika kipindi cha mwezi mmoja uliopita limekamata vitu na vielelezo mbalimbali ikiwemo Bangi pamoja na pikipiki za wizi.

Hayo yamebainishwa na kamanda wa jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga Kamishna Msaidizi wa polisi Janeth Magomi ambapo amesema jeshi hilo limeendelea kufanya doria na misako katika maeneo mbalimbali sanjari  na kutoa elimu kwa wananchi kupitia vyombo vya habari ili kuwajengea uelewa juu ya uhalifu.

Amesema jumla ya maderewa 6499 wa vyombo vya moto wametozwa faini ya makosa mbalimbali, wakiwemo madereva 6 wa magari wamepelewa mahakamani huku madereva watatu wakifungiwa leseni zao.

“Jumla ya madereva 6 wa magari walipelekwa mahakamini kwa makosa ya usalama barabarani, madereva 6499 wa vyombo vya moto walitozwa faini na pia madereva 3 walifungiwa leseni zao kwa upande wa mahakama jumla ya kesi 19 ziliweza kufanikiwa ambapo kesi 3 za makosa ya kubaka zilihukumiwa kifungo cha kati ya Miaka 30 hadi hadi kifungo cha maisha”.amesema Kamanda Magomi

Kamanda Magomi ametaja makosa mengine ya kesi mbalimbali zilizohukumiwa jela huku akitoa wito kwa wananchi kuendelea kufuata sheria za Nchi na kutojihusisha na vitendo vya kihalifu.

“Lakini pia kesi moja ya kulawiti ilihukumiwa kifungo cha maisha jela, kesi moja ya shambulio la aibu ilihukumiwa kifungo cha Miaka 20 jela na fidia ya shilingi Milioni moja, kesi tatu za wizi zilihukumiwa kifungo cha Mwaka mmoja jela, kesi moja ya ukatili dhidi ya mototo ilihukumiwa kifungo cha Miaka 3 jela pamoja na faini ya shilingi laki tano pia kesi moja ya kumtorosha mwanafunzi ilihukumiwa kifungo cha miaka 30 jela”.amesema Kamanda Magomi

“Vile vile kesi moja ya kughushi nyaraka ilihukumiwa kifungo cha miaka 5 jela, kesi moja ya wizi wa mototo ilihukumiwa kifungo cha miaka 3 jela, kesi 2 za wizi wa mifugo zilihukumiwa kifungo cha mwaka mmoja hadi 5 jela na pia kesi mbili za kujeruhi zilihukumiwa kifungo cha mwaka mmoja hadi 5 jela kezi zingine mbili za pikipiki zilihukimiwa kifungo cha miaka 2  jela na nyingine ya wizi ilihukumiwa kifungo cha miaka 6 jela na kulipa fidia ya shilingi milioni nane na kesi moja ya kupatikana na Bangi ilihukumiwa miaka miwili jela”.amesema Kamanda Magomi

“Tulifanikiwa kukamata jumla ya gramu 2205 pamoja na kete 61 za dawa za kulevya aina ya Bangi, pia tulikamata pikipiki 11, mifuko 24 ya cementi, ndoo 4 na makopo 4 ya rangi za nyumba, tulikamata Gypsum powder na vifaa mbalimbali vya ramli chonganishi”.

“Pia kutokana na ushirikiano mwema kati ya Polisi na jamii wananchi waliweza kutoa taarifa za uwepo wa aina ya silaha aina ya Pistol browning ikiwa na risasi 12 silaha hiyo iliweza kutelekezwa kwenye shule ya sekondari hapa Manispaa ya Shinyanga mtu aliitelekeza chooni mpaka sasa bado hatujampata mmiliki wake”.amesema Kamanda Magomi

Kuelekea sikukuu za krismas na mwaka mpya Jeshi la pilisI Mkoa wa Shinyanga limeendelea kujiweka katika hali ya utayari ili kukabiliana na vitendo mbalimbali vya kihalifu na kuhakikisha ulinzi wa raia na mali zao unaendelea kuimarika.

Kamanda wa jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga Kamishna Msaidizi wa polisi Janeth Magomi akitoa taarifa ya mananikio kwa waandishi wa habari katika misako na doria iliyofanyika kwa kipindi cha Mwezi mmoja.

This is received, thanks for your comments, will come back to you

Previous Post Next Post