HATARI-VITENDO VIPYA VYA UKATILI WA KIJINSIA VYAZIDI KUSHAMIRI NCHINI TANZANIA

 

Jedwali linaloonyesha ukubwa wa vitendo vya ukatili kwa miaka mitano 2018 hadi 2022  nchini Tanzania. source: www.nbs.go.tz

 *UBAKAJI WATAJWA KUWA KINARA WA MATUKIO YOTE


Ripoti ya Seif Mangwangi, Arusha


VITENDO vya ukatili wa kijinsia nchini Tanzania vimeendelea kushamiri jambo ambalo linazidi kuweka hatarini maisha ya wanawake na watoto ambao ndio wamekuwa wahanga wakubwa wa matukio hayo.


Kwa mujibu wa takwimu zilizotolewa na kuchapishwa na ofisi ya Taifa ya Takwimu ya Tanzania (NBS), makosa ya ubakaji yametajwa kuongoza kwa uhalifu dhidi ya binaadam kati ya matukio yote ambayo yameripotiwa katika jeshi la polisi nchini humo huku yakifuatiwa na mauaji ya binaadam.


Takwimu hizo zinaonyesha kwa kipindi cha miaka mitano, 2018 hadi 2022, jumla ya matukio 35849 ya ubakaji yameripotiwa kutokea nchini Tanzania sawa na asilimia 63 ya matukio yote kikiwa ni kiwango kikubwa kuwahi kutokea katika historia ya vitendo vya uhalifu wa aina hiyo nchini humo.


Makosa mengine ikiwemo mauaji ya binaadam, takwimu hizo ambazo zimekusanywa nchi nzima, zinaonyesha kuwa jumla ya matukio 12257 sawa na asilimia 21 yalitokea katika kipindi hicho ikiwa ni tofauti ya matukio 23,592 kati ya visa hivyo viwili vya ubakaji na mauaji.


Aidha takwimu zinaonyesha kwa kipindi hicho hicho matukio ya uhalifu wa makosa ya kushangaza (Un Natural Offence), yameshika nafasi ya tatu ambapo jumla ya visa 6771 viliripotiwa katika jeshi la Polisi.


Odero Charles Odero ni mwanaharakati wa haki za binaadam anayeishi katika jiji la Arusha, anasema moja ya sababu ya ongezeko la vitendo hivyo ni hali ngumu ya maisha ambayo huleta msongo wa mawazo na kujikuta wakitenda matukio hayo.


“Matumizi ya teknolojia na yenyewe yamekuwa yakisababisha vijana kufanya vitendo vya kikatili
hasa ubakaji wa watoto na wanawake lakini pia kulawiti,”amesema Odero Odero.


Kwa upande wake Wakili na Mwanaharakati wa haki za binaadam, Mary Mwita, anayeishi katika Jiji la Arusha, anasema mmomonyoko wa maadili katika jamii umekuwa ukichangia vitendo hivyo kushamiri kila siku licha ya kuwepo kwa sheria kali inayokataza matukio hayo.


https://storage.googleapis.com/gweb-newslab-data-viz-tool.appspot.com/uploads/720ffb1c-1858
-4eea-89cc-4ebc015528db.gif

Mary Mwita na Odero Odero wanashauri Ili kukomesha vitendo hivyo lazima suala la malezi liangaliwe upya na maisha ya ujamaa ambayo tumekuwa tukiishi zamani yarejeshwe kwa kila mtu katika jamii.

Dunia hivi sasa ipo kwenye siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia ambapo nchini Tanzania mashirika na taasisi mbalimbali ikiwemo umoja wa klabu za Waandishi wa Habari nchini humo (UTPC), ambapo wadau wamekuwa wakijadili mada mbalimbali kuhusu ukatili wa kijinsia.

This is received, thanks for your comments, will come back to you

Previous Post Next Post