MAMLAKA YA MAPATO TANZANIA (TRA) MKOA WA SHINYANGA YAFANIKIWA KUKUSANYA KODI BILIONI 32.8, WALIPA KODI WAPEWA ZAWADI NA VYETI VYA PONGEZI

Na Mapuli Misalaba, Shinyanga

Mamlaka ya mapato Tanzania (TRA) Mkoa wa Shinyanga imefanikiwa kukusanya kodi kiasi cha shilingi Bilioni 32.8 sawa na asilimia 82.21 ya lengo lililokusudiwa kwa Mwaka wa fedha 2022/2023.

Hayo yameelezwa  na Naibu mkurugenzi wa fedha TRA makao makuu Bi. Anna Mndeme kwenye kilele cha maadhimisho ya siku ya shukurani kwa mlipa kodi iliyofanyika katika viwanja vya zimamoto Nguzonane Manispaa ya Shinyanga

Amesema mafanikio hayo ni matokeo ya walipa kodi wazalendo na waandilifu wanaounga mkono juhudi za serikali katika kusukuma maendeleo.

“Kwa kuwa leo ni kilele cha maadhimisho ya siku ya shukurani nitumie nafasi hii kutambua mchango mkubwa wa wateja wetu yaani walipa kodi na wadau mbalimbali ambao ndiyo kipekee wanatuwezesha TRA Mkoa wa Shinyanga kufikia malengo ya makusanyo ya kodi tuliyopewa na serikali”.

“Mwaka wa fedha 2022/2023 mamlaka imefanikiwa kukusanya kodi kiasi ya cha Bilioni 32.8 ukusanyaji huu ni ufanisi wa asilimia 82.21 ya lengo la kukusanya ambalo tulipewa Mwaka huo”.

Katika maadhimisho hayo TRA Mkoa wa Shinyanga imewapongeza walipa kodi wote, kuwatambua na kuwatunuku vyeti na zawadi mbalimbali walipa kodi na wadau wengine ambao wameonyesha mchango mkubwa kwa mamlaka hiyo.

Afisa elimu na mawasiliano kwa mlipakodi Semeni Mbeshi ametaja baadhi ya majira ya washindi wa tuzo hizo ambapo kituo cha matangazo Radio Faraja FM kimeshinda tunzo katika nafasi ya chombo cha habari kinachosaidia kueneza zaidi elimu ya kodi kwa wafanyabiashara Mkoa wa Shinyanga.

 “Taasisi ya kwanza ambayo imeonyesha ushirikiano na TRA ni ofisi ya mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, ofisi nyingine ni ofisi ya RSO , ofisi nyingine ni ofisi ya kamanda wa jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga anayefuata ni vyombo vya habari  ambavyo vimeweza kuwa msaada katika kueneza masuala ya yetu ya kodi ikiwemo elimu ya kodi cheti kinaenda kwenye Redio ambayo inaitwa Redio Faraja”.amesema Semeni Mbeshi

Meneja wa TRA Mkoa wa Shinyanga Bwana Faustine Mdessa  amesema  katika maadhimisho hayo mamlaka hiyo  yamekwenda sanjari na kutoa msaada  kwa watu wenye uhitaji ikiwemo kituo cha wazee na wasiojiweza kolandoto pamoja na kutoa msaada wa Tenki la maji katika Hospitali ya Wilaya ya Kishapu.

Akizungumza mgeni rasmi kwa niaba ya mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Mkuu wa Wilaya ya Kahama Bi. Mboni Mhita ameipongeza TRA Mkoa wa Shinyanga kwa kutambua mchango wa walipakodi huku akiwakumbusha walipakodi kuendelea kulipa kodi kwa hiyari.

DC Mhita amewataka wafanyabiashara kutoa lisiti kwa kutumia mashine sahihi za EFD wakati wa mauzo huku akiwakumbusha wanunuzi kudai lisiti wakati wa kuchukua bidhaa kwa wafanyabishara hali itakayosaidia kuziba mianya ya ubotevu wa fedha.

Mstahiki meya wa Manispaa ya Shinyanga Elias Ramadhan Masumbuko na Mwenyekiti wa TCCA Mkoa wa Shinyanga Jonathan Manyama wamewaomba wakazi wa Mkoa wa Shinyanga  kuendelea kulipa kodi kwa hiyari.

Kauli mbiu ya maadhimisho hayo ni ‘KODI YETU. MAENDELEO YETU. TUWAJIBIKE’.

Awali yakiendelea matembezi ya hiyari kwa watumishi wa TRA, walipa kodi pamoja na wanafunzi wa klabu za kodi kutoka katika shule na vyuo mbalimbali Mkoani Shinyanga.








This is received, thanks for your comments, will come back to you

Previous Post Next Post