JUKWAA LA UWEZESHAJI WANAWAKE KIUCHUMI TANZANIA LATOA MSAADA HANANG'

 Na Mwandishi Wetu Manyara

JUKWAA la Uwezeshaji Wanawake Kiuchumi Tanzania limeipongeza Serikali  kwa namna ilivyojipanga katika kuwasaidia wananchi wa wilaya ya Hanang' mkoani Manyara waliokumbwa na tukio la Maporomoko  ya mawe na matope.

Akizungumza wakati wa kukabidhi misaada mbalimbali ya vitu vilivyotolewa na viongozi wa kitaifa kwa niaba ya Jukwaa hilo,  Makamu Mwenyekiti wa JUKWAA, Bi Joyce Ndosi  amesema jambo hilo limeleta faraja kubwa Kwa waathirika wa maporomoko hayo.

Naye Katibu Mkuu wa Jukwaa hilo Dkt. Regina Malima ameupongeza Uongozi wa Mkoa wa Manyara kwa utaratibu mzuri uliowekwa wa kupokea misaada inayotolewa na wadau mbalimbali nchini.

Kwa upande wake Mkuu wa mkoa wa Manyara Mh. Queen Sendiga  amelishukuru Jukwaa la  Uwezeshaji Wanawake Kiuchimi Tanzania kwa kuwakumbuka wananchi na hasa wanawake wenzao na watoto waliokumbwa na janga hilo.

Misaada  iliyotolewa na Jukwaa hilo ni  pamoja na Nguo, mikeka, Kanga, Vitenge, batiki na Sabuni.

Tukio la Maporomoko ya mawe na matope lilitokea Disemba 3, 2023 Katika Mji wa Kateshi wilayani Hanang' na kusababisha vifo na majeruhi ikiwemo kuathiri nyumba na miundo mbinu mbalimbali katika maeneo hayo.

This is received, thanks for your comments, will come back to you

Previous Post Next Post