JUMLA YA WATOTO 11 WAMEZALIWA KATIKA MKESHA WA SIKUKUU KITUO CHA AFYA KAMBARAGE NA HOSPITALI YA RUFAA MKOA WA SHINYANGA

Na Mapuli Misalaba, Shinyanga

Jumla ya watoto 11 wamezaliwa katika mkesha wa sikukuu ya Krismasi katika Hospitali ya rufaa ya Mkoa wa Shinyanga na kituo cha afya Kambarage mjini Shinyanga.

Watoto wanne wamezaliwa katika Hospitali ya rufaa ya Mkoa wa Shinyanga na saba katika kituo cha afya Kambarage.

Katika maelezo yake afisa muuguzi wa Hospitali ya rufaa ya Mkoa wa Shinyanga Experantia Misalaba amesema wanawake watatu wamejifungua kwa njia ya kawaida na mmoja amejifungua kwa njia ya upasuaji na kwamba wote wako salama.

Kwa upande wake muuguzi mkunga wa zamu kituo cha afya Kambarage Judith Masalu amesema kati ya wanawake 20 wajawazito waliolazwa katika kituo hicho saba kati yao wamejifungua kwenye mkesha wa Krismasi.

Amesema kati ya watoto saba waliozaliwa wanne ni watoto wa kiume na watoto wa kike ni watatu ambapo amesema mtoto mmoja amezaliwa chini ya uzito unaotakiwa.

Baadhi ya  akina mama waliojifungua katika mkesha wa Krismasi wamepongeza  huduma nzuri ambazo wameendelea kupatiwa na madaktari na wauguzi.

  

Afisa muuguzi wa Hospitali ya rufaa ya Mkoa wa Shinyanga Experantia Misalaba akizungumza leo Jumatatu Disemba 25,2023.


This is received, thanks for your comments, will come back to you

Previous Post Next Post