WAAMINI WAADIVENTISTA WASABATO SHINYANGA MJINI WAMUAGA MCHUNGAJI WAO LAZARO MBOGO BAADA YA KUHAMISHWA UTUMISHI

Na Mapuli Misalaba, Shinyanga.

Waamini  Waadiventista Wasabato Shinyanga mjini  Jumamosi Disemba 9,2023 wamemuaga mchungaji wao  Lazaro Mbogo baada ya kuhamishwa utumishi wake kwenda  mtaa wa Katungulu Sengerema Mkoani Mwanza.

Sabato maalum ya kumuaga Mchungaji huyo imefanyika katika eneo la kanisa la Waadiventista Wasabato Shinyanga mjini na kwamba, Mchungaji Mbogo amefanya utumishi wake kwa muda wa takribani Miaka mitatu akiwa anatoa mafundisho  na huduma mbalimbali za kiroho kwa upendo na furaha bila kuchoka.

Wakimuelezea mchungaji Mbogo waamini Waadventista  wasabato wamesema kuwa alikuwa  mlezi mzuri ambaye alikuwa mstari wa mbele katika kuchochea maendeleo na  kuwaimarisha kiimani.

Wamesema wataendelea kumuenzi na kuyaishi yale mema na mazuri  aliyokuwa akiyafundisha kwao,na hivyo kumtakia matashi mema na utumishi uliotukuka kule aendako kadri ya mapenzi ya mwenyezi Mungu.

Kwa upande wake mchungaji Lazaro Mbogo ametumia nafasi hiyo kuwashukuru waamini waadventista wasabato wa kanisa hilo, kwa ushirikiano wao na maombezi katika utumishi wake kwa kipindi chote ambacho amekuwepo pamoja nao.

Hata hivyo mchungaji Mbogo amewaasa kuendelea kutoa ushirikiano kwa mrithi wake atakayekuja kuchukua nafasi yake, na kuwashukuru kwa zawadi walizompatia kwani ni sehemu ya upendo mkubwa waliouonyesha kwake.

Waamini waadventina wasabato  Jumamosi Disemba 09 mwaka 2023 wamemshukuru mungu kwa ajili ya zawadi ya mchungaji lazaro mbogo katika kuwalea, kuwaongoza na kuwafundisha misingi ya imani, ambapo wamemzawadia vitu mbalimbali ikiwemo nguo,chakula na fedha.

 

Mchungaji  Lazaro Mbogo wa pili kutoka upande wa kulia na viongozi mbalimbali wakiwa katika mabato maalum ya kumuaga mchungaji huyo  Jumamos Disemba 9,2023.



This is received, thanks for your comments, will come back to you

Previous Post Next Post