Mwenyekiti wa Bodi ya shule za St Marys Dallas Mhoja akimpa cheti na zawadi ya fedha taslim Makamu mkuu wa shule ya St Mary’s Mbezi Beach, Rajab Balele kwenye hafla hiyo |
Mwenyekiti wa Bodi ya shule za St Marys Dallas Mhoja akimpa cheti na zawadi ya fedha taslim Makamu mkuu wa shule ya St Mary’s Mbezi Beach, Rajab Balele kwenye hafla hiyo |
Picha ya pamoja na wanafunzi waliofanya vizuri |
Na Mwandishi Wetu
WANAFUNZI waliomaliza kidato cha nne kwenye shule ya sekondari St Mary’ s Mbezi Beach na kufaulu kwa daraja la kwanza wamepewa zawadi mbalimbali kama motisha kwa wanafunzi wengine kuendelea kufanya vizuri kitaaluma.
Hafla ya kuwapongeza wanafunzi hao ilifanyika jana kwenye maeneo ya shule hiyo, Mbezi Beach na kuhudhuriwa na wazazi na wanafunzi waliomaliza kidato cha nne.
Zawadi walizopewa wanafunzi hao ni pamoja na fedha taslim, nguo za michezo pamoja na vitabu mbalimbali vya kitaaluma.
Akizungumza kwenye hafla hiyo, Makamu Mkuu wa shule hiyo, Rajab Balele, alisema mwaka 2020 walimu waliahidi kuleta mageuzi makubwa na walipambana usiku na mchana na kufanikiwa kupata matokeo mazuri.
Alisema wanafunzi 106 wa shule hiyo walihitimu kidato cha nne mwaka jana na miongoni mwao, wanafunzi 29 walipata daraja la kwanza, daraja la II wanafunzi 35 wanafunzi 13 daraja la tatu na kwamba hakuna aliyepata sifuri.
“Walimu kwa kushirikiana na wanafunzi wamefanyakazi kubwa sana usiku na mchana kuwa wabunifu kufundisha mpaka wanafunzi wengi kufaulu kwa alama za juu,” alisema na kuongeza.
“Nilipopata matokeo yetu ya kidato cha nne kwa kweli nilichanganyikiwa kwasababu sikuwa natarajia kwamba tutafaulisha kwa kiwango kikubwa namna hii, tulilahidi kufanya vizuri lakini matokeo yamekuwa mazuri sana kuliko nilivyotarajia,” alisema.
Balele aliwataka wanafunzi hao wasibweteke na badala yake waendelee kufanya vizuri kwenye elimu ya kidato cha tano na sita ili kupata alama zitakazowawezesha kujiunga na vyuo vikuu bila vikwazo.
“Kuna wakati shule ilikuwa hadi daraja 0 wanafikia wanafunzi 62 lakini kwa sasa hakuna division 0, na daraja la kwanza wameongezeka huu ndo mwaka tumefanikiwa kupata divisheni one nyingi kuliko mwaka wowote,” alisema na kuongeza.
“Kuna kufaulu na kufaulu sana, kwa hiyo ukiangalia matokeo yetu ya mwaka huu darala la kwanza za kiwango cha juu tumezipata nyingi na huo ndio utakuwa mwendo wetu tutahakikisha hakuna daraka 0 miaka yote na daraja la kwanza zitaendelea kuongezeka,” alisema.
Mkuu wa Taaluma wa shule hiyo, Shadrack Mgaya, alisema wanafunzi wa shule hiyo wamekuwa wakifanya vizuri kwenye mashindano mbalimbali ya kitaaluma.
Alisema mafanikio ya wanafunzi yanategemea pembe tatu ambazo ni Mwalimu, Mwanafunzi na Mzazi ambapo kila mmoja anapotimiza wajibu wake matokeo yanakuwa mazuri kama ambayo shule hiyo imepata kwa kidato cha nne.