Na Mapuli Kitina Misalaba
Waandishi wa habari wa Mkoa wa Shinyanga wameipongeza na kuishukuru Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) Kanda ya Magharibi kwa kuhitimisha mafunzo yao kwa vitendo.
EWURA kanda ya Magharibi ilianza kutoa mafunzo kwa waandishi wa habari Mkoa wa Shinyanga siku ya jana ambapo leo Ijumaa Aprili 3,2024 imehitimisha mafunzo yake kwa kufanya ziara ya kutembelea na kufahamu mambo mbalimbali, katika mradi mkubwa wa kusambaza majisafi kutoka Ziwa victoria hadi miji ya Kahama na Shinyanga (KASHWASA) uliopo Ihelele Wilaya ya Misungwi Mkoani Mwanza.
Waandishi wa Habari waliotembelea katika mradi huo wameipongeza na kuishukuru EWURA kwa ubunifu huo ambao umelenga kuwaimarisha katika utekelezaji wa majukumu yao hasa wakati wa kuripoti habari za Nishati na Maji.
Wameahidi kutumia vema kalamu zao katika kuhabarisha wananchi huku wakiziomba mamlaka zingine kutoa mafunzo kwa waandishi wa habari ili waweze kuendelea kuripoti habari zao kwa weledi kwa lengo la kutengeneza taifa bora.
Akizungumza meneja wa EWURA Kanda ya Magharibi Mhandisi Walter Christopher amewasisitiza waandishi wa habari kuendelea kuripoti habari zenye uhalisia ili wananchi wapate ueleza zaidi kuhusiana na upatikanaji wa maji na matumizi yake.
Mhandisi Christopher pamoja na mambo mengine ameelezea umuhimu wa ziara hiyo kwa waandishi wa habari Mkoa wa Shinyanga ambapo amesema EWURA kanda ya Magharibi itaendelea kushirikiana na waandishi wa habari kutoka Shinyanga Press Club (SPC).
“Tumefanya haya mafunzo kuanzia jana leo tumefanya ziara kwahiyo mafunzo haya ni muunganiko wa mafunzo ambayo tulianza kuyafanya jana ambayo tulielezana kinagaubaga kazi ambazo EWURA inafanya majukumu ambayo EWURA inafanya na tuliona katika sekta hizi mbali ambazo tunazidhibiti za Nishaji na Maji na tuliona kwenye sekta ya maji mamlaka ambazo tunazidhibiti ziko mamlaka 12 kama tulivyoelezana jana moja wapo ni mamlaka ya Maji KASHWASA”.
“Tuliona ni vizuri kutembelea mradi wa maji KASHWASA kwa sababu unavitu vingi kwanza maji yenyewe yanatoka ziwani na ziwa Victoria ni ziwa kubwa na maji yanaenda kwenye Mikoa mingi kwahiyo tukaona wakija hapa watajifunza mambo mengi ambayo yanahusiana na kazi ambazo tunazifanya sisi kama EWURA kwahiyo nashukuru sana kwa kutupokea ninaimani kwa waandishi wa habari hasa wanachama wa Shinyanga Press Club mmejifunza mambo mengi ambayo yanahusiana na shughuli za usambazaji wa huduma za Maji, na tunaimani baada ya kutoka hapa mtakuwa mnatoa habari ambazo nizauhakika zinauhalisia katika jamii”. Amesema Mhandisi Christopher
Meneja huduma kwa wateja KASHWASA John Ngano akizungumza.
Waandishi wa Habari Mkoa wa Shinyanga pamoja na Mamlaka ya kudhibiti huduma za Nishati na Maji EWURA Kanda ya Magharibi wakisikiliza maelezo namna maji yanavyozalishwa na kutibiwa kutoka ndani ya Ziwa Victoria.
Waandishi wa Habari Mkoa wa Shinyanga pamoja na Mamlaka ya kudhibiti huduma za Nishati na Maji (EWURA) Kanda ya Magharibi wakiangalia namna maji yanavyotibiwa ili yawe salama.
Waandishi wa Habari Mkoa wa Shinyanga pamoja na Mamlaka ya kudhibiti huduma za Nishati na Maji (EWURA) Kanda ya Magharibi wakiangalia namna maji yanavyotibiwa ili yawe salama.
Waandishi wa Habari Mkoa wa Shinyanga pamoja na Mamlaka ya kudhibiti huduma za Nishati na Maji (EWURA) Kanda ya Magharibi wakiangalia namna maji yanavyotibiwa ili yawe salama.
Makamu Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa Habari mkoa wa Shinyanga, Bw. Patrick Mabula akiishukuru na kuipongeza Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) Kanda ya Magharibi kwa ubunifu huo.