KUELEKEA MAADHIMISHO YA MIMEA DUNIANI TPHPA NA WADAU WENGINE WAJIPANGA.

Mwenyekiti wa Bodi ya Afya ya Mimea na Viuatilifu Tanzania Profesa. Alfred Temu akizungumza na Vyombo vya Habari Jijini Arusha

Egidia Vedasto 

Arusha

Mamlaka ya Afya ya Mimea na Viuatilifu Tanzania (TPHPA) kwa kushirikiana na Wadau wengine wamejipanga kuendana na kasi ya ukuaji wa Sekta ya kilimo Nchini.

Hayo yamezungumzwa na Mwenyekiti wa Bodi ya Afya ya Mimea na Viuatilifu Tanzania Profesa Alfred Temu kwa vyombo vya habari katika maandalizi ya Maadhimisho ya Siku ya Mimea Duniani yanayotarajiwa kufanyika  Jijini Arusha Mei 12 mwaka huu.

Profesa Temu amesema Mamlaka hiyo kwa kushirikiana na wadau wa kilimo wanatakiwa kuelimisha jamii kwa upana juu ya afya ya mimea kuwa ndio msingi wa tija wa sekta hiyo kwa kuendana na kasi ya ukuaji wa teknolojia duniani.

Dr. Neduvoto Mollel kutoka Kitengo cha Uhifadhi Bioanuai ya Mimea Tanzania

Aidha ameeleza kwamba uzalishaji wa hekta za kilimo cha umwagiliaji umeongezeka hadi kufikia hekta 836,000, na kueleza kuwa Mamlaka imejipanga kwa teknolojia ya ukaguzi mipakani katika usafirishaji wa nafaka kuhakikisha hakuna kisumbufu kinachoingia wala kutoka.

"Katika maadhimisho haya tunategemea kuungana na wadau mbalimbali wakiwemo wanasayansi wanaotengeneza na kuzalisha mbegu, wanaofungasha na kutawanya viuatilifu, Sekta binafsi, vyama vya wakulima na watawanya sumu(agro dealers)" amesema Profesa Temu.

Kwa Upande wake Kaimu Mkurugenzi wa TPHPA Dkt. Mujuni Kabululu, amesema dhumuni la maadhimisho hayo ni kufanya kilimo chenye tija katika mazingira salama na yanayotunzwa.

"Katika maadhimisho hayo tutaonyesha matumizi ya teknolojia katika umwagiliaji kwa kutumia mashine za kisasa za umwagiliaji ambazo pia zinaweza kudhibiti na kutambua viuatilifu na kutoa taarifa za uwepo wa visumbufu mahali fulani" amefafanua Dkt. Kabululu.

Pia Dkt. Neduvoto Mollel kutoka Kitengo cha Taifa cha Uhifadhi Bioanuai ya Mimea, ameeleza kwamba Tanzania inaongoza kwa kuwa na mimea mingi Afrika ikiongozana na Nchi Afrika Kusini na Congo.

Tunafanya kazi ya kuorodhesha aina zote za mimea na majina yake kwa faida ya vizazi vijavyo, na kwa ajili ya uhifadhi" ameongeza Dkt.Mollel.

Watendaji wa Kampuni ya Bens Agrostar Kanda ya Kaskazini wanaohusika na kuuuza na kusambaza pembejeo wakizungumza na mteja katika banda lao la maonyesho (katikati) ni Meneja Mauzo Kanda Salum Chutto

Hata hivyo, Meneja Mauzo Kanda ya Kaskazini kutoka Kampuni ya Bens Agro star inayojihusisha na kusambaza na uuzaji wa pembejeo, Salum Chutto amesema kuwa wamekuwa wakitoa mafunzo kwa wakulima namna bora ya kutumia pembejeo hizo ili wapate mazao mengi na kujikwamua kiuchumi.

sambamba na hayo Chutto amesema kwamba wanazingatia ubora katika bidhaa zao Kama njia ya kulinda Afya ya Mimea.

Maadhimisho ya Mwaka huu yamebeba Dhima inayosema, Afya ya mimea, biashara salama na teknolojia kidigitali.


This is received, thanks for your comments, will come back to you

Previous Post Next Post