MBUNGE WA VITI MAALUM MHE. SALOME MAKAMBA APIGA KURA KITUO CHA BUGWETO A JIMBO LA SHINYANGA MJINI KATIKA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA

 

 Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Shinyanga, Mhe. Salome Makamba, leo amepiga kura katika kituo cha Bugweto A, kilichopo Kata ya Ibadakuli, Jimbo la Shinyanga Mjini, kwa ajili ya uchaguzi wa viongozi wa serikali za mitaa.

Mhe. Makamba ameungana na wananchi wengine ikiwemo familia yake kushiriki katika zoezi hilo muhimu ambalo linaendelea kote nchini kwa lengo la kuchagua viongozi watakaowakilisha jamii kwenye ngazi za msingi.

Uchaguzi wa serikali za mitaa ni miongoni mwa hatua muhimu za kidemokrasia, zinazotoa fursa kwa wananchi kushiriki moja kwa moja katika maamuzi ya maendeleo ya maeneo yao.

Kwa sasa, zoezi la upigaji kura linaendelea katika vituo mbalimbali, huku usimamizi wa uchaguzi ukifanyika kwa kuzingatia kanuni na taratibu zilizowekwa na mamlaka husika.



 Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Shinyanga, Mhe. Salome Makamba akiwa kwenye foleni pamoja na familia yake wakati wa kwenda kupiga kura.

This is received, thanks for your comments, will come back to you

Previous Post Next Post