Na Mapuli Kitina Misalaba
Ligi ya Makamba Lameck (Krismas Cup 2024) inaendelea kwa kasi kwenye Uwanja wa Mhangu, Kata ya Salawe, Wilaya ya Shinyanga Vijijini.
Leo Jumanne Disemba 10, 2024 Mwasenge FC wameonyesha uwezo wa hali ya juu baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Mahando FC, na hivyo kufanikiwa kutinga hatua ya nusu fainali.
Msimamizi wa ligi hiyo, Mwalimu Emmanuel Enock Kijida, amethibitisha kuwa kesho Salawe FC watakutana na Mwabenda FC katika mechi ya robo fainali.
“Kwa matokeo ya leo, Mwasenge FC anasubiri mshindi wa mechi ya kesho ili kukutana naye katika hatua ya nusu fainali,” amesema Mwalimu Kijida.
Kwa mujibu wa ratiba, mechi za nusu fainali zitaanza siku ya Alhamisi, ambapo Beya FC watakutana na Kano FC ambapo Ijumaa itakuwa zamu ya Mwasenge FC kupambana na mshindi wa mechi ya kesho.
Fainali ya ligi hiyo imepangwa kufanyika Desemba 17, huku mechi ya mshindi wa tatu ikitarajiwa kuchezwa siku ya Desemba 16.
Mwalimu Kijida ametoa wito kwa wananchi na wadau wa michezo kufika kwa wingi kushuhudia ligi hiyo ya kipekee, akisema, “Ni fursa nzuri ya kukuza vipaji vya wachezaji wetu wa Shinyanga na maeneo jirani ikiwa ni pamoja na kuchochea maendeleo ya michezo.”
Ligi ya Krismas Cup 2024 inadhaminiwa na Makamba Mussa Lameck kupitia kampuni yake ya MCL inayojihusisha na biashara ya nafaka. Dhamira kuu ya ligi hiyo ni kuinua vipaji vya michezo na kuchangia maendeleo ya jamii mkoani Shinyanga.
Msimamizi wa ligi hiyo ya Krismas CUP, Mwalimu Emmanuel Enock Kijida, akizungumza.
Msimamizi wa ligi hiyo ya Krismas CUP, Mwalimu Emmanuel Enock Kijida, akizungumza.