BREAKING NEWS: MAXENCE Mello wa Jamii Forum aibuka mshindi tuzo ya Mwangosi 2019

Mkurugenzi Mkuu wa Jamii Forums Maxence Mello (kushoto) akipokea mfano wa hundi ya shilingi milioni 10 baada ya Jamii Forums kuibuka mshindi wa Tuzo ya Daudi Mwangosi 2019 kutoka kwa Balozi wa Sweden nchni,Anders Sjoberg katika ukumbi wa Rahaleo, Zanzibar,wa kwanza kulia ni Mkurugenzi wa UTPC, Abubakar Karsan

 KUTOKA ZANZIBAR
Mkurugenzi Mkuu wa Jamii Forums Maxence Mello, ameibuka mshindiwa tuzo ya Mwangosi mwaka 2019, kutokana na umahiri aliouonyesha katika tasnia ya habari kwa kipindi cha mwaka jana.

Tuzo hiyo hutolewa kila mwaka na Umoja wa Vilabu vya Waandishi wa Habari Tanzania(UTPC) kumkumbuka Daudi Mwangosi aliyeuawa akiwa kazini Septemba 2, 2012 kijijini Nyololo mkoa wa Iringa akitekeleza majukumu yake ya kikazi

Mwangosi ambaye alikuwa Mwenyekiti  wa Chama cha Waandishi wa Habari mkoa wa Iringa aliuwawa na Askari wa jeshi la Polisi kikosi cha kutuliza ghasia baada ya kudaiwa kurushiwa bomu.







Balozi wa Sweden nchini Tanzania,Anders Sjoberg akimkabidhi tuzo ya Daudi Mwangosi,Mkurugenzi  Mtendaji wa Jamii Media inayomiliki Mtandao wa Jamii Forums, Maxence Mello leo katika ukumbi wa Raha Leo,Zanzibar .
Mkurugenzi  Mtendaji wa Jamii Media inayomiliki Mtandao wa Jamii Forums, Maxence Mello akiangalia tuzo.
Mkurugenzi  Mtendaji wa Jamii Media inayomiliki Mtandao wa Jamii Forums, Maxence Mello akionesha  tuzo ya Daudi Mwangosi 2019.
Mkurugenzi  Mtendaji wa Jamii Media inayomiliki Mtandao wa Jamii Forums, Maxence Mello akionesha  tuzo ya Daudi Mwangosi 2019.

Balozi wa Sweden nchini Tanzania,Anders Sjoberg akimkabidhi hundi ya shilingi milioni 10 Mkurugenzi Mtendaji wa Jamii Media inayomiliki Mtandao wa Jamii Forums, Maxence Mello kwa kushinda tuzo ya Daudi Mwangosi 2019.
Mkurugenzi  Mtendaji wa Jamii Media inayomiliki Mtandao wa Jamii Forums, Maxence Mello akipokea hundi ya shilingi milioni 10 ambayo ni zawadi ya Tuzo ya Daudi Mwangosi 2019.

This is received, thanks for your comments, will come back to you

Previous Post Next Post