Mahakama ya Iran yamhukumu kifo jasusi wa CIA

Msemaji wa Idara ya Mahakama nchini Iran Bw. Gholam Hossein Esmaili, amesema Mahakama Kuu ya nchi hiyo imemhukumu kifo raia mmoja wa Iran ambaye ni jasusi wa Shirika la Upelelezi la Marekani, CIA.

Shirika la habari la Iran Fars limemnukuu Bw. Esmaili akisema kuwa, Amir Rahimpour, ambaye alikuwa mpelelezi wa CIA, alipewa kiasi kikubwa cha pesa ili kutoa baadhi ya taarifa kuhusu mpango wa nyuklia wa Iran kwa idara ya ujasusi ya Marekani.

Ameongeza kuwa watu wengine wawili wamehukumiwa kifungo cha miaka 10 kila mmoja gerezani kwa tuhuma za kufanya upelelezi kwa ajili ya Marekani.

This is received, thanks for your comments, will come back to you

Previous Post Next Post