Waliokuwa
wajumbe wa kamati ya utekelezaji wa makubaliano iliyosainiwa tarehe
22,Agosti ,2019 kati ya jeshi la zimamoto na uokoaji na kampuni ya ROM
Solutions Co.LTD leo Feb.5,2020 wamewasili ofisi za Taasisi ya kuzuia
na kupambana na Rushwa [TAKUKURU]makao makuu jijini Dodoma kwa ajili ya
kuhojiwa kutokana na kashfa ya kufanya mkataba mbovu wa Trilioni Moja
bila kupitishwa na bunge.
Idadi
ya wajumbe waliofika katika ofisi hizo leo ni sita ambapo walifika
ofisi za TAKUKURU pamoja na kompyuta mpakato [Laptop]walizopewa na
kampuni ya ROM SOLUTIONS CO.LTD.
Wajumbe
hao pia walikuwa wakilipwa posho za vikao USD 800 na kampuni hiyo
wakati wakiwa wanakutana katika vikao vyao vya majadiliano.
Wajumbe
hao ni pamoja na Kamishna wa zimamoto Mbaraka Semwanza,Naibu Kamishna
wa zimamoto Fikiri Salla,Naibu Kamishna wa Zimamoto Lusekelo Chaula’.
Wengine
ni Naibu Kamishna zimamoto Ully Mburuko,Mchumi zimamoto Boniface
Kipomela na Mchumi wa jeshi hilo la zimamoto na uokoaji Felis Mshana.
Ikumbukwe
kuwa sakata hilo la mkataba mbovu wa Trilioni moja limesababisha
aliyekuwa waziri wa Mambo ya ndani ya nchi Kangi Lugola kuachishwa
wadhifa huo na kuteuliwa mwingine hivi karibu George Simbachawene.