Hayo
ameyabainisha leo Februari 5, 2020, Bungeni Dodoma, wakati akijibu
swali la Mbunge wa Viti Maalum, Tauhida Gallos, lililohoji umuhimu wa
kufunga CCTV Camera katika vituo vya polisi, zitakazomuwezesha Mkuu wa
Kituo kufuatilia na kujua ni nini kinachoendelea kituoni.
"Jeshi
la Polisi halina bajeti ya kuwezesha ufungaji wa CCTV Camera vituoni,
hivyo Wabunge mshirikiane na wadau ili Camera hizo zinunuliwe zifungwe
na kupunguza malalamiko ya huduma isiyo na weledi ya askari kwa
wananchi" amesema Mhandisi Masauni.