Polisi Mererani ktk kashfa, wadaiwa kugawana mali za mtuhumiwa, ni mjane aliyebambikiziwa kesi ya wizi

Askari Polisi katika kituo Cha Polisi Mererani wilayani Simanjiro Mkoani Manyara wamelalamikiwa Kwa kupoteza Mali za mshtakiwa wakidaiwa kugawana katika mazingira ya utata na zingine kuzibadilisha na kumwekea mali chakavu.

Mkazi wa Mererani Furaha Lazaro(45)ambaye ni mfanyabiashara wa duka katika mji mdogo wa Mererani amewalalamikia polisi wa kituo hicho Kwa uonevu waliomfanyia kwa kukamata Mali zake wakimtuhumu kushirikiana na wezi jambo ambalo si kweli na kisha kugawana Mali zake.

Furaha amemwomba Rais Samia Suluhu na Mkuu wa Polisi Nchini IGP Simon Siro kumsaidia kuweza kupata Mali zake yakiwemo magodoro yaliyokuwa yanashikiliwa na polisi baada ya kumalizika kwa kesi yake mahakamani ameze kuendelea na biashara yake na kutunza familia yake kwani Kwa sasa anaishi Kwa shida na yeye ni mjane.

Akiongea Kwa masikitiko huku akibubujikwa na machozi mama huyo alidai kukamatiwa Mali zake na polisi wakituo hicho Desemba 9,2019 na kuchukuliwa magodoro 15 mapya ,Jenereta 1,Mtungi mmoja wa Gesi,Sabufa na spika 2,Tajiri mbili na Rimu zake mbili vyote vikiwa na thamani ya sh,milioni 3,370,000.

Alisema mara baada ya kufikishwa kituoni hapo pamona na bidhaa zake aliambiwa kuwa anatuhumiwa kushirikiana na waizi hivyo bidhaa hizo ni Mali ya wizi.
Furaha Lazaro


Alidai kuwa mkuu wa kituo hicho, aliyefahamika kwa jina moja la Makala aliamrisha apelekwe mahabusu na asipatiwe dhamana hadi uchunguzi utakapo kamilika,Jambo ambalo lilimshangaza wakati dhamana ni haki ya mshtakiwa.

"Nilikaa mahabusu siku sita Bila dhamana nilikuwa nikijaribu kuhoji mlalamikaji ni nani aje kutambua Mali yake ,lakini askari hao walikuwa wakinikejeri Kwa kuniambia si unanifanya mjanja"alisema.

Alieleza kuwa baada ya siku sita mkuu wa kituo hicho alilegeza masharti na kukubali dhamana ambapo mtuhumiwa huyo aliachiwa Kwa dhamana.

Alisema baada ya kutoka mahabusu aliamua kuwatafuta baadhi ya Wafanyabiashara wenzake alikokuwa akinunua bidhaa hiyo na walipofika kituoni ili kuthibitisha Mali hizo waliambulia kupigwa na kuswekwa rumande wakidaiwa ni wezi.

"Niliendelea kufuatilia Mali zangu na baada ya mwezi kupita nilienda Tena kituoni hapo lakini chaajabu nilipofika mkuu wa kituo aliamrisha nikamatwe na kupelekwa kituo Cha polisi wilaya ya Simanjiro"alisema.

Mjane alidai kuwa baada ya kufikishwa kituo Cha polisi cha wilaya ya Simanjiro aliwekwa tena mahabusu siku 16 na baadaye alipelekwa mahakamani na kusomewa kosa la wizi.

"Katika kipindi chote hicho nilikuwa nikiwahoji polisi mlalamikaji wa kesi hii ni nani lakini hakuna jibu walilokuwa wakinipatia na sikuwahi kumwona mlalamikaji yoyote akijitokeza kutambua Mali yake "alisema.

Alidai baada ya kufikishwa katika mahakama hiyo kesi ilikuwa ikitajwa bila mlalamikaji na baadaye ilifutwa lakini polisi walimkamata na kumfungulia kesi nyingine.

"Kesi ilifutwa Kwa zaidi ya mara tatu lakini polisi waliendelea kunitengenezea kesi nyingine na kunifikisha katika mahakama hiyo"alisema.

Mjane huyo alidai kuwa alilazimika kutumia gharama nyingi kusafiri kutoka Mererani kwenda Makao makuu ya wilaya ya Simanjiro yaliyopo Komolo kufuatilia kesi yake ambayo anadai alibambikiwa na polisi Kwa lengo la kumdhoofisha kibiashara baada ya kuwa akiwagomea kuwapatia chochote pindi walipokuwa walifika dukani kwake.

Alisema mnamo Machi ,25 mwaka huu kesi hiyo ilimalizika baada ya mahakama kumtaka kulipa kiasi cha sh,500,000 Kwa kosa ambalo hadi Sasa hafahamu ,fedha ambayo alichangiwa na ndugu zake.

Alisema baada ya kumalizika Kwa shauri hilo alianza tena kufuatilia mali zake ambapo polisi walimkabidhi magodoro chakavu tofauti ya Yale waliyokuwa wameyakamata awali ambayo ni mapya ,pia baadhi ya Mali zingine zilikuwa hazionekani Jambo lililomlazimu kutopokea Mali hizo.

"Nimekuwa nikifuatilia Mali zangu Kwa kamanda wa polisi Mkoa wa Manyara Harrison Mwakyoma ,nimeenda Babati ofisini kwake zaidi ya mara tatu bila mafanikio mara nyingi amekuwa akiahidi kufuatilia na kunipiga kalenda na pindi ninapomrudia hakuna Jambo la maana "alisema.

Alisema Kwa Sasa amechoka kufuatilia badala yake amemwomba Rais Samia Suluhu na IGP Simon Siro kumsaidia kuweza kupata Mali zake Kwa kuwa amechoka kuonewa kwani hata mwili wake Kwa Sasa umekufa ganzi upande mmoja Kutokana na kulala kwenye sakafu yenye baridi Kwa muda mrefu bila kupewa dhamana katika mahabusu ya Wilaya ya Simanjiro.

Akiongelea tuhuma hizo mkuu wa polisi Mkoa wa Manyara Kamanda Mwakyoma alikiri kufahamu suala la mama huyo akidai kuwa amemwomba aje Babati ofisini ili ampatie majina ya askari walioshiriki kukamata Mali hizo ili afuatilie.

"Ni kweli huyu mama amekuwa akija ofisini kwangu ila Kama upo naye naomba umwambie aje ofisini kwangu anione niweze kufuatilia na ikiwezekana uje naye wewe mwandishi."Alisema Mwakyoma Kwa njia ya simu.

Hata hivyo Kamanda alipoulizwa kwanini ameshindwa kulipatia ufumbuzi suala hilo wakati amekiri Mjane huyo kufika ofisini kwake mara kadhaa, Mwakyoma aliendelea kusisitiza Kwa kumtaka.mama huyo kufika ofisini kwake hata Kama atakuwa hana nauli aweze kumtumia.

This is received, thanks for your comments, will come back to you

Previous Post Next Post